title : STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO
kiungo : STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO
STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO
Wakati pazia la Ligi Kuu ya Vodacom Tanzania Bara 2017-2018 likitarajiwa kufunguliwa rasmi kesho Agosti 27, mwaka huu kwa timu zote 16 kuingia viwanjani,Kampuni ya Michezo ya Bahati Nasibu Mtandaoni – BIKO imeidhamini Klabu ya Stand United ‘Chama la Wana’ shilingi milioni 100 kuanzia mwaka huu.
Akizungumza katika mkutano wa hadhara uliofanyika leo Ijumaa,Agosti 25,2017mjini Shinyanga, Mbunge wa Jimbo la Shinyanga Mjini Mheshimiwa Stephen Masele (CCM) alisema BIKO wameamua kuidhamini timu hiyo baada ya kuridhishwa na mwenendo wa timu hiyo.
“Baada ya Stand United kupoteza mwelekeo na wadhamini wake Kampuni ya Acacia kujiondoa katika udhamini,hivi sasa nimeamua kuwa msimamizi mkuu wa timu hii,nimetafuta udhamini mwingine,nimeiomba kampuni ya Kitanzania ya BIKO,imekubali kuwa wadhamini wakuu na imetupatia shilingi milioni 100 kwa mwaka huu”,alieleza Masele.
Mbunge huyo alisema ameamua kuwa msimamizi mkuu wa timu hiyo ili kuhakikisha kuwa timu hiyo inafanya vyema katika michezo mbalimbali.
Hivyo makala STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO
yaani makala yote STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/stand-united-chama-la-wana-yapata.html
0 Response to "STAND UNITED 'CHAMA LA WANA' YAPATA UDHAMINI WA MILIONI 100 KUTOKA KAMPUNI YA BIKO"
Post a Comment