Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam.

Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam.
kiungo : Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam.

soma pia


Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam.



Mhandisi wa Mahakama ya Tanzania, Khamadu Kitunzi akielezea teknolojia inayotumika kujenga jengo la kituo cha mafunzo cha mahakama leo jijini dar es salaam.

Kaimu jaji Mkuu wa Tanzania Prof. Ibrahim Hamis Juma (katikati) akiwa na Mwakilishi wa Benki ya dunia nchini, Bella Bird (kulia) na kulia ni jaji kiongozi wa mahakama kuu ya Tanznaia Mhe. Ferdinand Wambali walipotembelea ujenzi wa kituo cha mafunzo cha Mahakama leo jijini Dar es salaam

Picha ya pamoja mara baada ya mazungumzo.


Na Mohamed Ali-Mahakama.
MAHAKAMA ya Tanzania inakusudia kuanzisha kituo cha Mafunzo kwa ajili ya watumishi wake pamoja na wadau ili kuwaongezea ujuzi utakaosaidia kuboresha huduma zinazotolewa na Mahakama.


Kituo hicho kinachojengwa katika eneo la Mahakama ya Kisutu jijini Dar es salaam kitawaunganisha watumishi wa Mahakama na wadau katika mafunzo kwa njia ya video (video conferencing).


Akizungumzia Kituo hicho, Kaimu Jaji Mkuu wa Tanzania Mhe. Prof Ibrahim Hamis Juma amesema ujenzi wa kituo hicho ni sehemu ya Maboresho ya huduma za Mahakama ambacho pia wadau wa Mahakama watakuwa ni sehemu ya mafunzo yatakayokuwa yakitolewa.


Amesema badala ya Majaji, Mahakimu, watumishi na wadau wa Mahakama kwenda kupata baadhi ya mafunzo kwenye chuo cha Uongozi wa Mahakama- Lushoto (IJA), baadhi ya mafunzo watakuwa wakiyapata katika kituo hicho.


Naye Mratibu wa Mpango Mkakati wa Mahakama pamoja na maboresho ya Huduma za Mahakama Mhe. Zahara Maruma alisema ujenzi wa kituo hicho ni utekelezaji wa nguzo ya tatu ya mpango Mkakati wa miaka mitano wa Mahakama ya Tanzania ambapo kupitia nguzo ya pili ya Mpango huo, Majaji na Mahakimu hupatiwa mafunzo mbalimbali ili kurahisisha upatikanaji wa haki kwa wakati.


Akizungumzia nguzo ya tatu ya Mpango huo, Mhe. Maruma alisema nguzo hiyo inahusiana na urejeshaji wa imani ya wananchi kwa Mahakama na ushirikishwaji wa wadau katika shughuli za Mahakama ambapo kupitia kituo hicho wadau wa Mahakama watahusishwa kwenye Mafunzo mbalimbali ili kurahisisha suala la upatikanaji wa Haki.


Kuhusu suala la matumizi ya Teknolojia ndani ya Mahakama, Mratibu huyo alisema hivi sasa Mahakama inao mpango wa kujenga vituo vya aina hiyo kwenye maeneo mbalimbali nchini kwa lengo la kuunganisha Mahakama zote nchini kwa njia ya video (video conferencing).


Ujenzi wa kituo cha Mafunzo cha Mahakama ulioanza hivi karibuni kwa ushirikiano kati ya Mahakama ya Tanzania na Benki ya Dunia unatarajiwa kugharimu kiasi cha shilingi za kitanzania milioni 78. Aidha, Jengo la kituo hicho cha mafunzo linajengwa kwa kutumia teknolojia ya gharama nafuu iitwayo Moladi na linatarajiwa kukamilika ndani ya wiki nane.


Hivyo makala Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam.

yaani makala yote Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/sheria-mahakama-kuanzisha-kituo-cha.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Sheria : Mahakama Kuanzisha kituo cha Mafunzo Dar es Salaam."

Post a Comment