title : PAMBANO LA MAYWEATHER NA MC GREGORL LAZIDI KUZUA GUMZO DUNIANI
kiungo : PAMBANO LA MAYWEATHER NA MC GREGORL LAZIDI KUZUA GUMZO DUNIANI
PAMBANO LA MAYWEATHER NA MC GREGORL LAZIDI KUZUA GUMZO DUNIANI
Kamali iliyochezwa katika Casino kubwa ya Las Vegas mwishoni mwa wiki imevunja rekodi na kuwa kubwa kiasi cha mifumo ya kuchezea kamali ya ‘sportsbook’ kushindwa kuhimili.
Kwa mujibu wa Espn, mtu mmoja ambaye ‘alibet’ mwishoni mwa wiki aliweka historia kwa kuweka dau la dola za Kimarekani laki nane na themanini elfu ($880,000) akisimamia kuwa Mayweather atampiga McGregor katika pambano lao litakalofanyika Agosti 26 mwaka huu katika ukumbi wa T-Mobile Arena nchini Marekani.
Hiki ni kiasi kikubwa zaidi cha fedha kuwahi kuwekwa kwenye kamali kwa mkupuo katika historia ya michezo ya masumbwi.
Kwa mujibu wa ‘bet’ hiyo, kama Mayweather atampiga McGregor, mtu huyo ‘aliyebet’ atajipatia faida ya dola za Kimarekani laki moja na sitini elfu ($160,000).
Dau hilo la kamali liliripotiwa kwa mara ya kwanza na Vegas Stats & Information, ambayo ilituma picha ya tiketi yake kwenye mitandao ya kijamii.
Hata hivyo, tiketi hiyo ilionesha kwa makosa kuwa mcheza kamali angepata faida ya $120,000 badala ya kiasi sahihi cha $160,000, kutoka na mfumo kushindwa kuhimili tarakimu hizo kwani mfumo hauruhusu kutoa jumla ya zaidi ya dola milioni moja, kwa mujibu wa Mkurugenzi wa ‘Sportsbook’, Chris Andrew. Hii ina maanisha $880,000 + $120,000 ndio mwisho wa tarakimu zinazokubalika kwenye mfumo huo.
Andrews amesema kwa namna ambavyo mfumo huo ulivyo, malipo yanayompa nafasi Mayweather yanapaswa kuwa dola za Kimarekani milioni moja ($1.04 million).
Hivyo makala PAMBANO LA MAYWEATHER NA MC GREGORL LAZIDI KUZUA GUMZO DUNIANI
yaani makala yote PAMBANO LA MAYWEATHER NA MC GREGORL LAZIDI KUZUA GUMZO DUNIANI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PAMBANO LA MAYWEATHER NA MC GREGORL LAZIDI KUZUA GUMZO DUNIANI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/pambano-la-mayweather-na-mc-gregorl.html
0 Response to "PAMBANO LA MAYWEATHER NA MC GREGORL LAZIDI KUZUA GUMZO DUNIANI"
Post a Comment