title : Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake
kiungo : Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake
Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake
WAENDESHAJI wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’, leo wamemkabidhi jumla ya Sh Milioni 20, mshindi wao wa droo ya 28, Moses Matagili, mkazi wa Goba, aliyetangazwa jana Jumatano, jijini Dar es Salaam.
Matagili anakuwa mshindi wa droo ya 28 ya Biko, inayochezwa kwa njia ya ujumbe mfupi wa maandishi kwa kufanya miamala kwenye simu za M-Pesa, Tigo Pesa na Airtel Money kuanzia Sh 1,000 na kuendelea, huku namba ya kampuni ikiwa ni 505050 na kumbukumbu ni 2456.
Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa fedha zake, Matagili anayejishughulisha na kazi za ujenzi wa nyumba, alisema amepokea ushindi wake kwa furaha, baada ya kuuwazia kwa muda mrefu na kuamua kuwa mchezaji mzuri wa Biko.
Alisema makabidhiano hayo ya fedha yamefanyika haraka, tofauti na matarajio yake, ikiwa ni siku moja baada ya kupigiwa simu ya ushindi na Balozi wa Biko, Kajala Masanja.
“Nashukuru kwa kushinda na kukabidhiwa fedha zangu mapema, nikiamini kuwa nitapiga hatua kubwa kiuchumi kwa namna moja ama nyingine, ukizingatia kuwa ndio matarajio yangu.
“Nawaomba Watanzania wote waendelee kucheza Biko mara nyingi zaidi na wasikate tamaa, kwa sababu kushinda kwangu kumeniongezea imani kubwa kwa waendeshaji wa Biko,” Alisema.
Moses Matagili mshindi wa Biko wa Milioni 20 mkazi wa Goba, katikati akipokea fedha zake kutoka kwa Mratibu wa Matukio na Mawasiliano wa Biko, Hassan Melles kulia, huku akishuhudiwa na afisa wa NMB, tawi na Bank House, jijini Dar es Salaam leo mchana.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA
Hivyo makala Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake
yaani makala yote Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/moses-matagili-akabidhiwa-milioni-20.html
0 Response to "Moses Matagili akabidhiwa Milioni 20 zake"
Post a Comment