title : Matukio : Kinana Amwandalia Balozi wa China Hafla ya Chakula cha Jioni Kumuaga
kiungo : Matukio : Kinana Amwandalia Balozi wa China Hafla ya Chakula cha Jioni Kumuaga
Matukio : Kinana Amwandalia Balozi wa China Hafla ya Chakula cha Jioni Kumuaga
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akimkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 2017. Hafla hiyo ilihudhuriwa na Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara, Rodrick Mpogolo, Naibu Spika Tulia Akson, Mabalozi kadhaa wanaoziwakilisha nchi zao hapa nchini, Mawaziri Kadhaa, Makatibu wa Sekretarieti ya Halmashauri Kuu ya Taifa na Makatibu wa Jumuia za Chama. Picha zote na Bashir Nkoromo.
Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing akimshukuru Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana baada ya kupokea zawadi maluum, ambayo Kinana alimzawadia wakati wa chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza kabla ya kumkabidhi zawadi maalum Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia), wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 2017.
Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia) akiifungua zawadi hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing (kulia) akizungumza wakati wa hafla hiyo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing wakiinua glasi za vinwaji kabla ya kuzigonganisha kutakiana heri, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson. Picha zote na Bashir Nkoromo.
Katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana akigonganisha glasi za viwanywaji na Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing kumtakia heri, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni alichomwandalia Balozi huyo kumuaga, Upanga jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 2017. Kulia ni Naibu Spika wa Bunge Tulia Akson. Picha zote na Bashir Nkoromo.
Balozi wa China nchini Tanzania Dk. Lu Youqing akigonganisha glasi za vinywaji na Spika wa Bunge Tulia Akson kutakiana her, wakati wa hafla ya Chakula cha jioni kilichoandaliwa na katibu Mkuu wa CCM Abdulrahman Kinana kumuaga Balozi huyo, Upanga jijini Dar es Salaam, Agosti 25, 2017. Kulia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu Uratibu wa Bunge
Naibu Katibu Mkuu wa CCM-Bara Rodrick Mpogolo akigonganisha Glasi na Balozi wa Zambia hapa nchini Judith Kangoma-Kapijimpanga wakati wa hafla hiyo.
Katibu wa Jumuia ya wanawake Tanzania Amina Makilagi, Katibu wa Halmashauri Kuu ya Taifa ya CCM Idara ya Uchumi na Fedha Dk. Frank Hawassi na kaimu Katibu Mkuu wa UVCCM Shaka hamdu Shaka wakiwa na glasi za vinywaji vyao wakati wa hafla hiyo.
Hivyo makala Matukio : Kinana Amwandalia Balozi wa China Hafla ya Chakula cha Jioni Kumuaga
yaani makala yote Matukio : Kinana Amwandalia Balozi wa China Hafla ya Chakula cha Jioni Kumuaga Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Matukio : Kinana Amwandalia Balozi wa China Hafla ya Chakula cha Jioni Kumuaga mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/matukio-kinana-amwandalia-balozi-wa.html
0 Response to "Matukio : Kinana Amwandalia Balozi wa China Hafla ya Chakula cha Jioni Kumuaga"
Post a Comment