title : FAIDA YA SERIKALI KUGHARAMIA ELIMU BURE NI WANAFUNZI KUFAULU–PROFESA NDALICHAKO.
kiungo : FAIDA YA SERIKALI KUGHARAMIA ELIMU BURE NI WANAFUNZI KUFAULU–PROFESA NDALICHAKO.
FAIDA YA SERIKALI KUGHARAMIA ELIMU BURE NI WANAFUNZI KUFAULU–PROFESA NDALICHAKO.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia , Profesa Joyce Ndalichako akizindua mabweni mawili katika Shule ya Sekondari Nasibugani iliyopo Wilaya ya Mkuranga.
Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako akipanda mti katika shule ya Sekondari Nasibugani
.Mkurugenzi wa Halmashauri ya Mkuranga, Mshamu Munde akizungumza wananchi na wanafunzi katika shule ya Sekondari Nasibugani.
Na Chalila Kibuda , Globu ya Jamii.
SERIKALI inatoa sh. bilioni 18.77 kwa ajili ya kugharamia elimu bure ili kila mtanzania apate elimu bora ili wanafunzi wanafaulu darasa la Saba na Kidato cha Nne na kuendelea na elimu ya kidato cha tano na hadi chuo kikuu.
Hayo ameyasema leo Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Profesa Joyce Ndalichako wakati wa uzinduzi mabweni katika shule ya sekondari Nasibugani ambayo ujenzi wake uko katika hatua ya mwisho pamoja na Shule ya Sekondari Mwinyi ambayo ujenzi umekamilika kwa kuingia wanafunzi katika mabweni hayo wilayani Mkuranga mkoani Pwani.
Profesa Ndalichako amesema serikali ya awamu ya tano imeondoa gharama katika shule ya msingi na sekondari ili kuondosha mzigo kwa wazazi ambao walikuwa wanashindwa kugharamia elimu hiyo.
Amesema mabweni yaliyojengwa katika shule ya sekondari Nasibugani na Mwinyi zenye Kidato cha Kwanza hadi Sita ni kuongeza sehemu ya kumwezesha mwanafunzi kusoma kwa muda mrefu na kuweza kondokana na vishawishi vinavyopatikana mtaani.
Aidha amesema kuwa serikali itaendelea kuboresha shule na makazi ya walimu yaliyo bora pamoja na huduma zingine ikwemo umeme katika shule ya Sekondari Nasibugani. pia Mkuranga iko nyuma kielimu ni ukweli usiofichika hivyo walimu pamoja na watendaji kuhimiza suala la elimu ili viwanda vilivyopo na wanamkuranga wanufaike na sekta hiyo.
Waziri Profesa Ndalichako amempongeza Mbunge wa Mkuranga Abdallah Ulega kuanzisha Program kwa wanafunzi wa sekondari kuwa Hakuna Kufeli. Amesema Program hiyo ifanywe kwa vitendo kwa wanafunzi kujitoa zaidi kusoma kwani mtihani uko karibu lakini wakitumia program hiyo watafanya vizuri na kuondoa sifuri katika shule zao na kuanza daraja la kwanza hadi la tatu.
Hivyo makala FAIDA YA SERIKALI KUGHARAMIA ELIMU BURE NI WANAFUNZI KUFAULU–PROFESA NDALICHAKO.
yaani makala yote FAIDA YA SERIKALI KUGHARAMIA ELIMU BURE NI WANAFUNZI KUFAULU–PROFESA NDALICHAKO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala FAIDA YA SERIKALI KUGHARAMIA ELIMU BURE NI WANAFUNZI KUFAULU–PROFESA NDALICHAKO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/faida-ya-serikali-kugharamia-elimu-bure_15.html
0 Response to "FAIDA YA SERIKALI KUGHARAMIA ELIMU BURE NI WANAFUNZI KUFAULU–PROFESA NDALICHAKO."
Post a Comment