DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO

DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO
kiungo : DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO

soma pia


DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO


NA K-VIS BLOG/Khalfan Said

KAIMU Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (pichani), amewataka Wahandisi Wanawake wa Shirika hilo, kutembelea mashuleni ili kuwahamasisha (Motivate), wanafunzi wa kike ili wapende kujisomea masomo ya sayansi na Hisabati na hatimaye baadaye waje kushika nafasi kama walizo nazo wao.

Dkt. Mwinuka ameyasema hayo makao makuu ya TANESCO jijini Dar es Salaam, wakati akiwapongeza Wahandisi wanawake wa Shirika hilo, baada ya kupewa tuzo na Makamu nwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe. Samia Suluhu Hassan, kwa kuibuka wakwanza kwenye Kongamano la Wahandisi wanawake Tanzania “Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition, (TAWECE), ambalo huenda sambamba na maonesho ya shughuli za kihandisi lililofanyika hivi karibuni jijini Dar es Salaam.

“Niwapongeze sana kwa kuibuka washindi wa kwanza kwenye maonesho hayo, lakini niwaase, mpatapo nafasi mtembelee mashuleni ili muwahamasishe wanafunzi wasichana kupenda kusoma masomo ya sayansi na hisabati, na kwa kupitia kwenu, wanaweza kujitokeza wasichana wengi kupenda masomo hayo na hivyo baadaye kufanya kazi za kihandisi kama nyinyi.” Alisema Dkt. Mwinuka.

Dkt. Mwinuka alisema, tuzo hiyo ni heshima kubwa kwa Shirika kwani inajenga picha (image) nzuri mbele ya jamii kuonyesha juhudi zetu za kuwahudumia wateja wetu. Alisema.

Akizungumza kwa niaba ya wenzake kwenye hafla hiyo fupi, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, alisema Wahandisi wanawake kutoka TANESCO, walionyesha umahiri wao katika kuelezea teknolojia ya usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre), inayotumia kuboresha huduma wanazozitoa katika jamii.
Kaimu Mkurugenzi Mtendaji wa Shirika la Umeme Tanzania, (TANESCO), Dkt. Tito Mwinuka, (kushoto), akipokea kikombe (tuzo), kutoka kwa Mwakilishi wa Wahandisi wanawake kutoka Shirika hilo, Mhandisi Rosamystica Lutenganya, katika hafla fupi iliyofanyika makao makuu ya Shirika hilo jijini Dar es Salaam Agosti 25, 2017.

 Wahandisi wanawake wa TANESCO walikabidhiwa tuzo hiyo na Makamu wa Rais, baada ya kuibuka wa kwanza kwenye kongamano na maonesho linalowakutanisha wahandisi wanawake kutoka sekta mbalimbali hapa nchini lijulikanalo kama "Tanzania Women Engineers Convention and Exhibition-TW=AWECE". Wahandisi hao walionesha umahiri mkubwa jinsi wanavyoweza kutumia teknolojia ya kisasa katika usimamizi wa miundombinu ya usambazaji umeme (Distribution Control Centre) inayotumika kuboresha huduma.
Dkt. Mwinuka, akiwapongeza baadhi ya wahandisi hao.
Dkt. Mwinuka akizungumza wakati wa hafla hiyo.



Hivyo makala DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO

yaani makala yote DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/08/dkt-mwinuka-awapongeza-wahandisi.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DKT. MWINUKA AWAPONGEZA WAHANDISI WANAWAKE TANESCO, KWA KUPEWA TUZO"

Post a Comment