title : Wizara ya Maliasili na Utalii yapokea msaada wa mil. 940 kusaidia kupambana na ujangili
kiungo : Wizara ya Maliasili na Utalii yapokea msaada wa mil. 940 kusaidia kupambana na ujangili
Wizara ya Maliasili na Utalii yapokea msaada wa mil. 940 kusaidia kupambana na ujangili
Taasisi ya Kimataifa ya Kijamii ya Uhifadhi wa Wanyamapori (WCS) imetoa msaada wa zaidi ya shilingi milioni 940 ambazo zimetumika kujenga ofisi, kununua vitendea kazi yakiwemo magari na kughamaramia mafunzo kwa askari wa wanyamapori wa mapori ya akiba ya lukwati- piti ili kukabiliana na ujangili na uwindaji haramu ambao umesababisha vifo vya tembo wapatao 23 tangu mwaka 2013 mpaka sasa.
Meneja wa mapori hayo ya akiba ya lukwati/ piti Alphonce Ambroce Mung’ong’o amesema mapori hayo mawili yenye ukubwa wa zaidi ya kilomita za mraba 6,119 yaliyoko Lupa Tingatinga mkoani Songwe yanatumika kwa uwindaji wa kitalii wa wanyamapori ambayo katika kipindi cha miaka mitano iliyopita yameiingizia serikali mapato ya zaidi ya dola za kimarekani milioni 1.3 sawa na zaidi ya shilingi bilioni mbili na milioni mia nane na amewaonya watu wanaojihusisha na ujangili kuwa sasa watafute kazi nyingine:
Akiongea katika hafla ya kukabidhi miradi hiyo ikiwemo jengo la kisasa, magari na vifaa vya doria kwa serikali ya Tanzania, Mkurugenzi wa WCS, Aaron Nicholaus amesema WCS inajivunia kushirikiana na serikali ya Tanzania katika kuimarisha uhifadhi.
Pia amezungumzia umuhimu wa mapito ya wanyamapori ambayo yameathiriwa na shughuli za binadamu licha ya umuhimu wake kwa uhifadhi ambapo katibu mkuu wizara ya maliasili na utalii meja jenerali gaudance milanzi amesema msimamo wa serikali katika uhifadhi uko wazi kwani maliasili hizo zina umuhimu kwa maendeleo ya taifa.
Kaimu Mkurugenzi mkuu wa mamlaka ya wanyamapori tanzania tawa, martin loibooki amesema tawa inatambua wajibu wake na malengo ya kuanzishwa kwa mamlaka hiyo ya kusaidia kuchochea maendeleo ya jamii na kukuza uchumi wa nchi kupitia sekta ya wanyamapori na ameishukuru wcs kwa kuwa mfadhili wa kwanza kufadhili shughuli za uhifadhi katika mapori ya lukwati- piti
Hivyo makala Wizara ya Maliasili na Utalii yapokea msaada wa mil. 940 kusaidia kupambana na ujangili
yaani makala yote Wizara ya Maliasili na Utalii yapokea msaada wa mil. 940 kusaidia kupambana na ujangili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Wizara ya Maliasili na Utalii yapokea msaada wa mil. 940 kusaidia kupambana na ujangili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/wizara-ya-maliasili-na-utalii-yapokea.html
0 Response to "Wizara ya Maliasili na Utalii yapokea msaada wa mil. 940 kusaidia kupambana na ujangili"
Post a Comment