title : TANAPA YATOA TUZO YA HESHIMA YA UTUNZAJI WA SOKWE KWA DKT. JANE GOODALL
kiungo : TANAPA YATOA TUZO YA HESHIMA YA UTUNZAJI WA SOKWE KWA DKT. JANE GOODALL
TANAPA YATOA TUZO YA HESHIMA YA UTUNZAJI WA SOKWE KWA DKT. JANE GOODALL
Na Karama Kenyunko, Globu ya Jamii.
Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Shirika la Hifadhi za Tanzania TANAPA, limempatia tuzo nne za Heshima, mwanasayansi na mtafiti wa kimataifa Dkt. Jane Goodall. Dkt. Jane amekabidhiwa tuzo mapema leo na Waziri wa Maliasili na Utalii Prof. Jumanne Magembe ambazo ni kinyago cha Sokwe, Kitenge, cheti cha heshima na ngao.
Tuzo hiyo ya heshima imetolewa maalumu kwa kutambua mchango wake katika masuala ya utafiti na uhifadhi wa Sokwe kwenye hifadhi ya taifa ya Gombe ambao ameufanya kwa zaidi ya miaka 60. Akizungumza wakati wa hafla ya utoaji tuzo hizo, Waziri wa Magembe amesema, Tanzania ni nchi ya kwanza ya uhifadhi katika bara Africa.
Katika hifadhi zetu za taifa za wanyama mbali mbali ambazo ziko 16, ziko pia, hifadhi za taifa mbili, Gombe na Mahale ambazo wanyama wanaohifadhiwa humo kwa sehemu kubwa ni Sokwe ambapo hata katika dunia hizo mbili ndio hifadhi nzuri kupita zote.
Amesema, Kazi kubwa iliyofanywa na mtafiti huyo imeiwezesha jamii kugundua kuwa, Sokwe, wanajitambua na kushirikiana. Wao kama wanyama, wana hisia zao kama viumbe na kama binadamu.
Amesema, kabla ya utafiti huo wa Sokwe, na katika ulimwengu wa sayansi binadamu ndio waliokuwa wa wanahisiwa kuwa ndio wenye hisia na kushirikiana kama viumbe wenye akili sana kumbe hata Sokwe kwani wao pia wanatumia nyenzo katika maisha yao.
Ameongeza kuwa tafiti anazofanya zimekusanya takwimu zenye maana kubwa sana katika uhifadhi wa Sokwe na pia katika uhifadhi wa wanyama pori. "Kwa mchango wake huu alioutoa, kidunia, kimataifa lakini kwa Tanzania kutoa mchango huu, tumeamua kumtunukia tuzo katika uhifadhi wa wanyamapori na zaidi Sokwe" amesema Waziri Maghembe.
Hivyo makala TANAPA YATOA TUZO YA HESHIMA YA UTUNZAJI WA SOKWE KWA DKT. JANE GOODALL
yaani makala yote TANAPA YATOA TUZO YA HESHIMA YA UTUNZAJI WA SOKWE KWA DKT. JANE GOODALL Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANAPA YATOA TUZO YA HESHIMA YA UTUNZAJI WA SOKWE KWA DKT. JANE GOODALL mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/tanapa-yatoa-tuzo-ya-heshima-ya.html
0 Response to "TANAPA YATOA TUZO YA HESHIMA YA UTUNZAJI WA SOKWE KWA DKT. JANE GOODALL"
Post a Comment