title : RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA
kiungo : RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA
RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mh.Paul Makonda amepokea Kompyuta 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 kutoka kwa kampuni ya ulinzi ya TAMOBA,ikiwa kama namna ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri unaofanywa na Ofisi hiyo.
Upatikanaji wa kompyuta hizo umekuja ikiwa ni sehemu ya shauku na utafutaji wa RC Makonda kwa ajili ya kuongeza tija na ufanisi katika kuwahudumia wananchi wa Dar es Salaam, ambapo itakumbukwa hivi karibuni Mh.Makonda alifanya mkutano na Watumishi wa sekta ya Ardhi wa Manispaa zote na moja ya kero kubwa iliyo bainishwa kuwasumbua wananchi ni namna ya kupata kibali cha ujenzi jambo lililomkera RC Makonda.
Kucheleweshwa kwa huduma ya namna hii kwa wananchi huchochea utoaji Rushwa na ujenzi holela bila vibali unaosababisha Serikali kupoteza kodi ya viwanja na kodi zingine zinazohusiana na ardhi.
Aidha amesema kuwa wananchi wamekuwa wakipata kero mbalimbali ikiwemo ile ya kupewa kibali na manispaa kisha wakaja watu wa zima moto wakakuzuia kuendelea kwa ujenzi sababu hawana taarifa, huku wakati mwingine ukimalizana na watu Zimamoto wanakuja watu wa OSHA nao wanakuzuia usiendelee na ujenzi.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda ( kushoto) akikabidhiwa Kompyuta 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 na Mkurugenzi wa kampuni hiyo, Joseph Kimisha, kulia ni Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa.
Baadhi ya Kompyuta hizo.Picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam,Paul Makonda (wakwanza kulia) akizungumza leo jijini Dar es Salaam katika hafla ya kukabidhiwa Computer 50 zenye thamani ya shilingi Million 85 na kampuni ya ulinzi ya TAMOBA kama sehemu ya kuunga mkono utendaji kazi mzuri
Makamu Mwenyekiti wa Bodi ya TAMOBA Balozi Mstaafu Francis Mndolwa kizungumza mchache katika hafla hiyo leo jijini Dar es Salaam.
Hivyo makala RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA
yaani makala yote RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/rc-makonda-apokea-kompyuta-50-zenye.html
0 Response to "RC MAKONDA APOKEA KOMPYUTA 50 ZENYE THAMANI YA SHILINGI MILLION 85 KUTOKA KAMPUNI YA TAMOBA"
Post a Comment