Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA.

Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA.
kiungo : Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA.

soma pia


Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA.

KATIBU Mtendaji wa Baraza la Sanaa Tanzania (BASATA) Geofrey Mngereza amekubali kuwa mgeni rasmi katika Tamasha la Wasanii litakalofanyika Ijumaa jijini Dar es Salaam.

Mwenyekiti wa Mtandao wa Wasanii Tanzania (SHIWATA),Cassim Taalib alisema Mngereza atashuhudia michezo mbalimbali itakayofanywa na wasanii na wanamichezo.

Alisema tamasha hilo ambalo awali lilikuwa lifanyike kijiji cha Wasanii Mkuranga limehamishiwa jijini Dar es Salaam sababu kubwa ya kuhamisha tamasha hilo ni kutokana na mvua ya msimu uliopita kuharibu barabara ya kwenda kijijini.

Taalib alisema tamasha hilo sasa litafanyika kwa siku mbili kuanzia Ijumaa Julai 14.7.2017 na kuhitimishwa Jumamosi Julai 15 mwaka huu katika viwanja vya Chuo cha Uhazili, splendid Ilala Bungoni.Alisema mpaka sasa wanatarajia kupokea wanamichezo kutoka sehemu mbalimbali kama vile Mkuranga, Kibiti, Zanzibar na Morogoro ambako zaidi ya wanamichezo 600 wamethibitisha kushiriki.

Baadhi ya michezo ambayo itafanyika ni sarakasi, Tae kwon-do, muziki wa dansi, ngumi, soka,rede,muziki wa asili,wu shuu,ngoma,singeli na michezo mingine.Alisema kampuni ya SBC wanaotengeneza soda za Pepsi imekubali kuwa wadhamini wakuu wa tamasha hilo na kuongeza kuwa milango iko wazi kwa wadhamini wengine kujitokeza.

Akizungumzia ujenzi wa nyumba zao kijijini alisema mgawo na makabidhiano ya nyumba 14 ndogo,kubwa tatu na viwanja 35 vilivyopimwa utafanyika Julai 16 siku moja baada ya kumalizika tamasha hilo.

Alisema kuanzia sasa wanachama wanaotaka kujenga nyumba zao wenyewe wawasiliane na Shiwata ili wapewe maelekezo na utaratibu wa kufanya usafi kwenye makazi yao.Mwenyekiti alisema utaratibu wa kulipia umeme kupitia mpango wa umeme vijiijini (REA)unaendelea na mikakati ya kukarabati barabara ya kufika kijijini unafanyika.


Hivyo makala Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA.

yaani makala yote Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/07/mngereza-kuwa-mgeni-rasmi-tamasha-la.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Mngereza kuwa mgeni rasmi tamasha la SHIWATA."

Post a Comment