title : ZIWA KITANGILI LAFUNGWA KWA MWAKA MMOJA KULINDA UOTO WA ASILI
kiungo : ZIWA KITANGILI LAFUNGWA KWA MWAKA MMOJA KULINDA UOTO WA ASILI
ZIWA KITANGILI LAFUNGWA KWA MWAKA MMOJA KULINDA UOTO WA ASILI
KAMATI za ulinzi na usalama za wilaya za Igunga,Meatu,Kishapau pamoja na Iramba zimelifunga ziwa kitangili kwa muda wa mwaka mmoja kuanzia julai,01,mwaka huu hadi Julai,01,2018 ili kulinusuru ziwa hilo lisitoweke,kulinda raslimali zilizopo na kulinda uoto wa asili ili uweze kurejea kutokana na uvuvi haramu unaoendelea katika ziwa hilo.
Mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama ya wilaya ya Iramba,Emmanueli Luhahula alitoa kauli hiyo kwenye mkutano wa baraza la Kawaida la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba uliofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo,uliopo mjini Kiomboi.
“Lakini pia Mwenyekiti nieleze suala la ziwa Kitangili ni mwendelezo ule ule wa Mkoa wetu kuwa jangwa na sisi tuliokabidhiwa wilaya tumefanya kikao cha kamati za ulinzi na usalama wilaya nne,wilaya ya Igunga,Meatu,Kishapu na Iraamba ambao wote tunafaidika na ziwa Kitangili”alifafanua Mwenyekiti huyo.
“Utakumbuka wewe mwenyewe Mwenyekiti ulifadhili kamati hii kwenda kujadili mara ya kwanza tukiwa na baadhi ya madiwani,lakini baadaye tulikubaliana kuu zenyewe zinazosimamia ulinzi tukakutane”alisisitiza Luhahula.
Kwa mujibu wa Luhahula baada ya kukutana Mkoani Shinyanga kutokana na hali halisi ya ziwa kitangili na kutokana na tathimini ya wataalamu iliyoletwa kuhusu ziwa hilo ikieleza kwamba likiachwa jinsi lilivyo kwa kipindi cha miaka kumi ziwa hilo litakuwa limetoweka.
Baadhi ya wakuu wa idara wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba wakiwa kwenye ukumbi wa mikutano wa Halmashauri hiyo wakati wa mkutano wa kawaida wa baraza la madiwani uliofanyika mjini Kiomboi.
Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba,Mkoani Singida,Simon Tyosela(wa kwanza kutoka kulia) akiongoza mkutano wa Baraza la Madiwani wa Halmashauri ya wilaya hiyo.(Picha zote Na.Jumbe Ismailly).
Hivyo makala ZIWA KITANGILI LAFUNGWA KWA MWAKA MMOJA KULINDA UOTO WA ASILI
yaani makala yote ZIWA KITANGILI LAFUNGWA KWA MWAKA MMOJA KULINDA UOTO WA ASILI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala ZIWA KITANGILI LAFUNGWA KWA MWAKA MMOJA KULINDA UOTO WA ASILI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/ziwa-kitangili-lafungwa-kwa-mwaka-mmoja.html
0 Response to "ZIWA KITANGILI LAFUNGWA KWA MWAKA MMOJA KULINDA UOTO WA ASILI"
Post a Comment