title : Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao
kiungo : Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao
Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao
NAIBU Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mheshimiwa Anthony Mavunde, amewataka Watanzania hususan wakazi na wananchi wa Dodoma kunufaika kiuchumi kwa kuutumia vyema uwapo wa mchezo wa bahati nasibu wa Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’.
Mh Mavunde ameyasema hayo jana wakati wa makabidhiano ya Sh Milioni 20 kutoka kwa mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, ambaye ni fundi cherehani mwenye maskani yake mjini Dodoma, akitangazwa mshindi katika droo ya 17.
Akizungumza katika makabidhiano hayo, Waziri Mavunde alisema kwamba serikali ya awamu ya Tano ni ya viwanda, hivyo ni jukumu la washindi hao kuhakikisha kwamba wanaanzisha na kusimamia biashara kubwa kwa kutumia mamilioni ya Biko.
Alisema fedha za Biko zinaweza kutumiwa vizuri na washindi wao, huku katika jimbo lake, mbali na watu kuibuka na ushindi wa papo kwa hapo unaonzia Sh 5,000, 10,000, 20,000, 50,000, 100,000, 500,000 na Sh Milioni moja zinazolipwa kwa kupitia simu za mikononi za kampuni za Tigo Pesa, M-Pesa na Airtel Money ambapo namba ya kampuni ya Biko 505050 na ile ya kumbukumbu ni 2456.
“Nawataka kila mtu ahakikishe kwamba akipata fedha hizi anazitumia vizuri na mimi kama mbunge wao wa Dodoma nitasimamia katika kuwapatia mwangaza mzuri wakati wowote wakihitaji, maana lengo la serikali ni kupiga hatua kiuchumi,” Alisema.
Naye Evodi Mlingi aliwapongeza Biko kwa kuhakikisha kwamba wamemfikishia fedha zake haraka tofauti na matarajio yake, licha ya kuwa na imani kubwa na waendeshaji wa mchezo wa Biko ambao umekuwa ukitoa fedha nyingi kwa washindi wao.
“Nimekuwa mchezaji mzuri wa Biko kila siku na kila saa ambapo ninapopokea fedha ya ushindi wa papo kwa hapo naipeleka tena Biko jambo ambalo nimepata ushindi mnono kwa kuchanganya na maombi yangu kwa Mungu, maana nina uhitaji mkubwa wa fedha na hizi nilizopata naahidi kuzipeleka kwenye fungu la kumi kama nilivyotaka tangu mwanzo,” Alisema Mlingi huku akiwashauri Watanzania kucheza kwa wingi ili wapate ushindi.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde, kulia akiwa na mshindi wa droo ya 17 ya Biko, Evodi Mlingi, baada ya kukabidhiwa fedha zake jana mjini Dodoma. Waziri Mavunde amepongeza mshindi huyo na kumtaka azitumie fedha zake kwa uangalifu ili afanikiwe kiuchumi.
Naibu Waziri wa Kazi, Vijana na Ajira, Mh Anthony Mavunde kulia akiwa na wananchi wake wa Dodoma Mjini walioshinda Sh Milioni 20 za Biko kila mmoja. Evodi Mlingi katikati amekabidhiwa fedha zake jana wakati kushoto ni Ramadhan Juma Hussein aliyeshinda Milioni 20 hivi karibuni ambapo tayari ameshapokea fedha zake kutoka Biko.
Hivyo makala Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao
yaani makala yote Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/waziri-mavunde-ataka-watu-watumie-biko.html
0 Response to "Waziri Mavunde ataka watu watumie Biko kukuza uchumi wao"
Post a Comment