title : Utalii : Waziri, Prof. Maghembe Amuaga Balozi wa Ujerumani Nchini anayemaliza muda wake
kiungo : Utalii : Waziri, Prof. Maghembe Amuaga Balozi wa Ujerumani Nchini anayemaliza muda wake
Utalii : Waziri, Prof. Maghembe Amuaga Balozi wa Ujerumani Nchini anayemaliza muda wake
Waziri wa Maliasili, Prof. Jumanne Maghembe (kushoto) akikabidhi zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori kwa Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Waziri Maghembe alimshukuru Balozi huyo kwa ushirikiano na misaada mbalimbali aliyoitoa, yeye binafsi na nchi yake katika kusaidia kuendeleza sekta ya uhifadhi nchini.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (katikati) akifurahia zawadi ya picha na vinyago vya wanyamapori alivyopewa na Waziri wa Maliasili na Utalii, Prof. Jumanne Maghembe (kulia) katika hafla ya kumuaga na kumshukuru iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous, mkoani Morogoro. Balozi huyo ataondoka nchini kesho Ijumaa, tarehe 23 Julai, 2017 kurudi nchini kwao Ujerumani. Kulia ni Katibu Mkuu, Wizara ya Maliasili na Utalii, Maj. Gen. Gaudence Milanzi.
Balozi wa Ujerumani nchini aliyemaliza muda wake, Egon Konchanke (kushoto) akizungumza katika hafla hiyo iliyofanyika hivi karibuni katika Pori la Akiba la Selous mkoani Morogoro.
Hivyo makala Utalii : Waziri, Prof. Maghembe Amuaga Balozi wa Ujerumani Nchini anayemaliza muda wake
yaani makala yote Utalii : Waziri, Prof. Maghembe Amuaga Balozi wa Ujerumani Nchini anayemaliza muda wake Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Utalii : Waziri, Prof. Maghembe Amuaga Balozi wa Ujerumani Nchini anayemaliza muda wake mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/utalii-waziri-prof-maghembe-amuaga.html
0 Response to "Utalii : Waziri, Prof. Maghembe Amuaga Balozi wa Ujerumani Nchini anayemaliza muda wake"
Post a Comment