Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki

Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki
kiungo : Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki

soma pia


Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki

Benny Mwaipaja, WFM, Dodoma

Pamoja na malalamiko na manung’uniko ya hali ngumu ya maisha kwa watanzania wengi, Tanzania ndio yenye kiwango cha chini cha mfumuko wa bei wa wastani wa asilimia 6.1 kwa mwezi Mei 2017 kwa nchi za Afrika Mashariki.

Hayo yamebainishwa leo bungeni Mjini Dodoma na Waziri wa Fedha na Mipango Dkt. Philip Mpango akiwasilisha Taarifa ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2016 na Mpango wa Maendeleo kwa mwaka 2017/18.

Mhe. Dkt. Mpango amesema mfumuko wa bei katika nchi za Afrika Mashariki kwa mwaka 2016 uliendelea kuwa wa kiwango cha tarakimu moja, ambapo Rwanda ilikuwa na asilimia 7.1, Uganda asilimia 5.4, Tanzania asilimia 5.2, Kenya asilimia 6.3 na Burundi asilimia 5.6.

Alisema kufikia mwezi Aprili 2017, mfumuko wa bei kwa nchi hizi ulipanda, ambapo kwa Burundi ulifikia asilimia 21.10, Rwanda asilimia 13.0; Kenya asilimia 10.28; Uganda asilimia 6.4 na Tanzania asilimia 6.4. 

“Hata hivyo, kwa upande wa Tanzania mfumuko wa bei umeendelea kushuka mpaka asilimia 6.1 kwa mwei Mei 2017” amesema Dkt. Mpango

Mhe. Dkt Mpango amesema kwa miaka minne mfululizo, wastani wa mfumuko wa bei kwa Tanzania umeendelea kupungua, ukibaki katika kiwango cha tarakimu moja.

Amesema kwa mwaka 2016, mfumuko wa bei ulifikia wastani wa asilimia 5.2 ikilinganishwa na asilimia 5.6 mwaka 2015. Kupungua kwa wastani wa mfumuko wa bei nchini kulichangiwa kwa kiasi kikubwa na: mwenendo wa kushuka kwa bei za mafuta ya petroli katika soko la dunia na nchini; kuimarika kwa upatikanaji wa vyakula nchini na hivyo kuimarisha wastani wa bei; na kuwepo kwa sera madhubuti za usimamizi wa bajeti na fedha.

Mhe. Dkt. Mpango amesema mfumuko wa bei uliongezeka kidogo, ambapo ulifikia asilimia 6.4 mwezi Aprili 2017 lakini ukiwa ndani ya maoteo ya wastani wa tarakimu moja (asilimia 5 – 8) kwa mwaka 2017.



Hivyo makala Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki

yaani makala yote Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/tanzania-yafanikiwa-kudhibiti-mfumuko.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Tanzania yafanikiwa kudhibiti mfumuko wa bei Afrika Mashariki"

Post a Comment