title : TANGAZAO MUHIMU: MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI
kiungo : TANGAZAO MUHIMU: MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI
TANGAZAO MUHIMU: MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI
Kiwanda cha Kuzalisha Viuadudu vya Kuua Viluwiluwi vya Mbu wa Malaria kilichopo Kibaha, Mkoani Pwani. |
Tarehe 22 June 2017, Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alilipia VIUADUDU vya kutokomeza Mbu wa Malaria lita 100,000 na kuagiza vigawanywe kwenye Halmashauri zote nchini.
Waziri wa Afya,Maendeleo ya Jamii,Jinsia,Wazee na Watoto Mhe Ummy Mwalimu anapenda kuwatanganzia Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini kuwa VIUADUDU hivi vitaanza kugawiwa leo kwa Halmashauri za Mikoa 14 yenye kiwango kikubwa cha Maambukizi ya Ugonjwa wa Malaria.
Mikoa hii (na kiwango cha maambukizi ya malaria kimeonyeshwa kwenye mabano) ni;- Kagera (41%), Geita (38%), Kigoma (38%), Ruvuma (23%), Tabora (20%), Mtwara (20%), Mara (19%), Morogoro (14%), Shinyanga (17%), Lindi (17%), Pwani (15%), Mwanza (15%), Katavi (14%) na Simiyu (13%).
Mikoa mingine ambayo haijatajwa itagawia Viuadudu katika Awamu ijayo. Idadi ya Lita zitakazogawanywa kwa kila Halmashauri zilizo katika Mikoa hii tayari imeshaainishwa.
Wizara inawakumbusha Waganga Wakuu wa Mikoa/Wilaya kufanya Upuliziaji wa Viuadudu kwa kuzingatia Miongozo ya Wizara ya Afya. Hii itawezesha kupata matokeo tarajiwa ya kutokomeza mbu ili kudhibiti ugonjwa wa Malaria nchini.
Aidha, Wizara ya Afya inapenda kumshukuru kwa dhati na kumpongeza Mhe.Rais Dkt. Magufuli kwa kuongeza chachu katika Mapambano dhidi ya Malaria Nchini.
Imetolewa na;
Catherine Sungura
Kaimu Msemaji- Idara Kuu Afya
26 June 2017
Hivyo makala TANGAZAO MUHIMU: MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI
yaani makala yote TANGAZAO MUHIMU: MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANGAZAO MUHIMU: MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/tangazao-muhimu-mgao-wa-viuadudu-vya.html
0 Response to "TANGAZAO MUHIMU: MGAO WA VIUADUDU VYA KUTOKOMEZA MBU WA MALARIA LITA 100,000 NCHINI"
Post a Comment