title : MANISPAA YA UBUNGO KUBORESHA SOKO LA SHEKILANGO
kiungo : MANISPAA YA UBUNGO KUBORESHA SOKO LA SHEKILANGO
MANISPAA YA UBUNGO KUBORESHA SOKO LA SHEKILANGO
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii.
MSTAHIKI Meya wa Manispaa ya Ubongo, Boniface Jacob amefanya kikao na wafanyabiashara wa Soko la Shekilango ili kuweka makubaliano ya maboresho ya soko hilo.
Maboresho hayo ambayo yamelenga kuliweka soko la Shekilango na masoko mengine ya Manispaa ya Ubongo katika hadhi nzuri na kuongeza mapato kwa serikali.
Akizungumza na wafanyabiashara katika soko hilo, Jacob amesema, maboresho ya soko hilo yametengewa Tsh milioni 50 ambazo ni mapato ya ndani ambayo yaliyotokana na kodi zao. Amesema maboresho hayo yataanza baada ya siku 7, yatachukua siku 14 kukamilika na wafanyabiashara waliopisha marekebisho hayo kurudi sehemu zao za biashara.
Jacob amesema mara baada ya wafanyabiashara kurejea katika maeneo yao, makubaliano ya ushuru yatakuwa baina ya Manispaa ya Ubungo na mfanyabiashara na siyo tena mfanyabiasha na mfanyabiashara.
"Nimekuja kuwasikiliza wafanyabiashara wote sitaki kuwaletea njaa,nataka tuangalie hali ya sasa na mzunguko wa ela tangu 2000 na tukubaliane".
Jacob amesema mara baada ya maboresho ya mabanda ya mbogamboga ambayo ushuru wake utapanda kidogo, awamu itayofuata itawagusa wapanga na wamiliki wa fremu 12 na vyoo ambao kwasasa wanalipa sh 200 kwa siku.
Aidha Jacob aliwataka wamiliki wa fremu hizo kwenda kwa Mkurugenzi wa Manispaa kufanya mazungumzo naye ili kupata makubaliano ya pamoja ya kisheria ili fremu hizo ziwe mali ya serikali na wao kulipia ushuru unaoendana na mahitaji ya sasa kiuchumi.
Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface Jacob akizungumza na wafanyabiashara wa Soko la Shekilango juu ya maboresho ya soko hilo leo jijini Dar es Salaam.
Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface Jacob akimununuza wafanyabiashara katika Soko la Shekilango alipotembelea soko hilo.
Mstahiki Meya wa Ubungo, Boniface Jacob akitembelea Soko la Shekilango juu ya kulifanyia maboresho leo jijini Dar es Salaam.picha na Emmanuel Massaka,Globu ya jamii.
Hivyo makala MANISPAA YA UBUNGO KUBORESHA SOKO LA SHEKILANGO
yaani makala yote MANISPAA YA UBUNGO KUBORESHA SOKO LA SHEKILANGO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MANISPAA YA UBUNGO KUBORESHA SOKO LA SHEKILANGO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/manispaa-ya-ubungo-kuboresha-soko-la.html
0 Response to "MANISPAA YA UBUNGO KUBORESHA SOKO LA SHEKILANGO"
Post a Comment