title : MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM
kiungo : MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM
MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM
NA K-VIS BLOG/Khalfan Said
MAFUNZO ya siku tano kwa madaktari yaliyoandaliwa na Mfuko wa Fidia kwa Wafanyakazi, (WCF), ili kuwajengea uelewa wa namna ya kufanya tathmini ya ugonjwa na ajali kwa mfanyakazi aliyepata madhara mahala pa kazi yamemalizika kwa washiriki kutunukiwwa vyeti.
Mafunzo hayo yaliyofunhga na Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba makao makuu ya Mfuko huo, jingo la GEPF barabara ya Bagamoyo jijini Dar es Salaam, Juni 23, 2017, yaliwaleta pamoja madaktari 70 kutoka hospitali mbalimbali za umma na binafsi jijini Dar es Salaam.
Mafunzo hayo yaliyogusa maeneo mbalimbali pia yaliwawezesha madaktari hao kujifunza Muongozo mpya unaohusu namna ya kufanya tahmini kabla ya kumlipa fidia stahiki Mfanyakazi aliepata madhara mahala pa kazi.
Akizungumza kwenye ufungaji wa mafunzo hayo, Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw Masha Mshomba, alisema kuwa ni iani ya Mfuko kuwa Madaktari hao wamefaifika na mafunzo hayo na yatawezesha ufanisi katika kjutoa huduma hizo kwa wafanyakazi waliopata magonjwa au kuumia wakati wakiwa kazini.
Mkurugenzi Mkuu wa WCF, Bw. Masha Mshomba, akimkabidhiDkt.Kezia, cheti cha ushiriki wa mafunzo ya tathmini ya ajali na majeraha kwa mfanyakazi aliyeumia wakati akitekeleza majukumu yake mahala pa kazi, wakati wa kilele cha mafunzo ya siku tano kwa madaktari kutoka hospitali za umma na binafsi za jijini Dar es Salaam. Jumla ya madaktari 70 kutoka hospitali 35 walishiriki.
Mkuu wa Kitengo cha Uhusiano WCF, Bi. Laura Kunenge, (kulia), akifuatilia kwa makini hafla hiyo ya ufungaji wa mafunzo kwa wataalamu hao wa afya.
Hivyo makala MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM
yaani makala yote MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/mafunzo-ya-siku-tano-kwa-madaktari_24.html
0 Response to "MAFUNZO YA SIKU TANO KWA MADAKTARI YALIYOANDALIWA NA WCF YAFUNGWA JIJINI DAR ES SALAAM"
Post a Comment