Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri

Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri
kiungo : Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri

soma pia


Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri

Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu imeridhia ombi la upande wa mashtaka la kutaka ushahidi utakaotolewa na askari polisi kutoka Makao Makuu ya Upelelezi wa Makosa ya Jinai Kitengo cha kupambana na Ujangili,D 7847 Sajenti Beatus usikilizwe kwa usiri.

Ushahidi huo ni katika kesi ya  uhujumu uchumi kwa kujihusisha na Meno ya Tembo ya bilioni 13 inayomkabili  raia wa China anayedaiwa kuwa Malkia wa Pembe za Ndovu, Yang Feng Glan (66)na watanzania wawili.

Mapema wakili wa Serikali Paul Kadushi, aliiomba Mahakama hiyo  ushahidi wa askari huyo ambaye awali alikwishaanza kutoa ushahidi wake kwa uwazi, usikilizwe kwa usiri kwa sababu unahusisha masuala ya amani ndani ya nchi.

Hakimu Mkazi Mkuu, Huruma Shaidi alikubaliana na ombi hilo la upande wa mashtaka kusikilizwa kwa usiri.

Hata hivyo, mmoja wa mawakili wa utetezi, wa Masumbuko Lamwai alilipinga hilo na kudai kuwa hakuna mahusiano juu ya Pembe za Ndovu na amani ya nchi.

Alidai kuwa, upande wa mashtaka hawakueleza ni kwa namna gani ushahidi wa Pembe za Ndovu utaingiliana na amani na utulivu katika nchi hii.

Aliongeza kuwa, mtu yoyote anayetuhumiwa kutenda kosa ni haki yake kikatiba,kesi isikilizwe hadharani ili kuhakikisha Haki ionekane imetendeka na umma ujue.

 Aliongeza kuwa kufanya hivyo kunaleta uwezekano wa mtu kuleta ushahidi wa kubambika.

Alibainisha kuwa upande wa mashtaka haujaweza kutoa sababu kwa nini ushahidi wa shahidi huyo uendelee kusikilizwa kwa usiri wakati ndugu wana Haki ya kujua hii kesi inaendeleaje.

" Kesi imekuwa kijamii mno, halafu isikilizwe kwa usiri kama mahakama ya kijeshi siyo Haki, mteja wangu amepewa Umalkia wa Pembe za Ndovu huo umalkia uthibitishwe hadharani siyo kisiri siri tunaomba hilo ombi likataliwe." Aliomba Lamwai.



Hivyo makala Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri

yaani makala yote Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/kesi-ya-meno-ya-tembo-ya-milioni-13.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Kesi ya meno ya Tembo ya Milioni 13 dhidi ya Raia wa China na Watanzania sasa kusikilizwa kwa usiri"

Post a Comment