Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa
kiungo : Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa

soma pia


Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa

 Na Karama Kenyunko, Globu ya jamii.

Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni na mfanyabiashara wamefikishwa katika Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kujibu mashtaka manne ya kuomba na kupokea rushwa.

Mwendesha Mashtaka kutoka taasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Emmanuel Jacob amewataja washtakiwa hao kuwa ni  Omary Mohammed Abdallah ambaye ni Hakimu na mfanyabiashara George Joseph Barongo.

Wakisomewa mashtaka yao mbele ya Hakimu Mkazi Respicious Mwijage, imedaiwa kuwa, kati ya January na Februari 12/ 2017 hakimu Omary alitenda kosa.

Imedaiwa kuwa, siku hiyo Omary akiwa muajiriwa wa Mahakama ya Mwanzo Kinondoni aliiomba rushwa  ya sh. 205,000 kutoka kwa Agnes Nyenza kwa ajili ya kumsaidia kwenye kesi yake ya mirathi ya namba 570/2016 ambayo ilikuwa mbele yake.

Katika shtaka la pili Hakimu Omary anadaiwa kupokea rushwa ya kiasi hicho cha fedha Kutoka kwa Nyenza ili aweze kumsaidia katika kesi hiyo.

Mahakama imeendelea kuambiwa kuwa, kati ya Februari na Machi mwaka huu, jijini Dar es salaam, Hakimu Omary akiwa na mfanyabiashara Barongo waliomba rushwa ya sh. Milioni moja kutoka kwa Nyenza kwa ajili ya kumsaidia katika kesi hiyo ya mirathi.

Wakili wa Takukuru aliendelea kuieleza mahakama kuwa, siku na mahali hapo watuhumiwa hao wote kwa pamoja walipokea rushwa ya sh. 500,000 kwa ajili ya kumsaidia Agnes Nyenza kwenye kesi yake ya mirathi ambayo iko mbele ya hakimu huyo Omary Mohammed wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni.

Hata hivyo washtakiwa wamekana kutenda kosa hilo na wako nje kwa dhamana hadi Julai 4 mwaka huu.


Hivyo makala Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa

yaani makala yote Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/hakimu-wa-mahakama-ya-mwanzo-magomeni.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Hakimu wa Mahakama ya Mwanzo Magomeni apandishwa kizimbani kwa rushwa"

Post a Comment