title : DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI
kiungo : DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI
DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Simon Berege ameupongeza mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS na kueleza kuwa mfumo huo ni suluhusisho la hati zenye mashaka katika halmashauri mbalimbali nchini.
Mfumo wa FFARS unatekelezwa katika mikoa 13 kwenye halmashauri 93 kwa ushirikiano wa serikali na mradi wa Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma ‘ Public Sector Systems Strengthening – PS3’ unaofadhiliwa na Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) pamoja na Mradi wa Tuimarishe Afya ‘ Health Promotion and System Strengthening – (HPSS) unaofadhiliwa na watu wa Uswizi (Swiss Tropical and Public Health Institute).
Akifungua mafunzo kuhusu mfumo huo kwa maafisa elimu kata na Waganga Wafawidhi katika vituo vya afya kutoka kata 18 za halmashauri ya Msalala,yaliyofanyika leo katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama,Berege alisema mfumo wa FFARS ni mwarobaini wa tatizo la halmashauri kupewa hati zenye mashaka.
Alisema mfumo huo utawezesha takwimu nyingi za halmashauri za wilaya kukusanywa kwa usahihi zaidi kutoka vituo vya kutolea huduma ambavyo vitakusanya na kuhifadhi taarifa za mapato na matumizi ya fedha za serikali kwa kutumia mfumo huo.
“Takwimu ni tatizo la kitaifa,hivyo mfumo huu utasaidia kuondoa tatizo hili kwa kuongeza uwazi na umakini katika masuala ya uhasibu na utoaji taarifa za fedha”,alieleza Berege. “Halmashauri zimekuwa zikipata hati zenye mashaka kwa sababu uwekaji takwimu haupo vizuri,FFARS ni tiba ya hati zenye mashaka,pamoja na kuendelea kutumia njia za vitabu/makaratasi,ni vyema halmashauri zikawa tayari kutumia njia za ki- elektroniki katika utunzaji takwimu”,aliongeza Berege.
Aidha alilishukuru Shirika la Maendeleo ya Kimataifa la Marekani (USAID) kwa kufadhili mradi huo na kuwataka watanzania kuutumia vizuri ili kuleta maendeleo katika halmashauri.
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga Simon Berege akifungua kuhusu mfumo mpya wa uhasibu na utoaji taarifa za fedha kwa ngazi ya kituo cha kutolea huduma ‘Facility Financial Accounting and Reporting System – FFARS kwa maafisa elimu kata na waganga wafawidhi katika vituo vya afya kutoka halmashauri hiyo leo Alhamis June 8,2017 katika ukumbi wa Submarine Hotel mjini Kahama
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akizungumza wakati wa kufungua mafunzo hayo
Mkurugenzi Mtendaji wa Halmashauri ya Msalala Simon Berege akifungua mafunzo hayo.Kushoto ni Mshauri wa kifedha kutoka PS3,Osoro Otieno,kulia ni Mratibu wa PS3 Halmashauri ya Msalala,Elikana Zabron .
Hivyo makala DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI
yaani makala yote DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/ded-msalala-mfumo-wa-uhasibu-na-utoaji.html
0 Response to "DED MSALALA: MFUMO WA UHASIBU NA UTOAJI TAARIFA - FFARS NI TIBA YA HATI ZA MASHAKA KWENYE HALMASHAURI"
Post a Comment