DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA

DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA
kiungo : DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA

soma pia


DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA

MKUU wa wilaya ya Ikungi mkoani Singida Miraji Mtaturu amewafuturisha waislamu wa wilaya hiyo huku akiwaasa kuendeleza tabia njema kwa mujibu wa kitabu cha Mwenyezi Mungu Quran hata baada ya mwezi Mtukufu wa Ramadhan kumalizika.

Akizungumza na waislamu hao baada ya kupata futuru wilayani humo Mtaturu alisema katika Mwezi Mtukufu wa Ramadhan watu wametenda mema yanayopaswa kuendeleza hata baada ya mwezi huo.

“Wakati tupo kwenye mfungo huu tupo kwenye darasa la tabia njema hivyo nawashauri hata baada ya mfungo huu tuyaendeleze,”alisema Mtaturu.Alisema serikali inafarijika pale inapoona wananchi wake wakifuata imani za dini zao na hivyo kuwa raia wema na nchi kuendelea kuwa na amani.

“Tunamaliza kukamilisha moja ya nguzo tano za uislamu panapo majaaliwa ya Mwenyezi Mungu,nawaombeni isiwe mwisho wa kufanya mema bali iwe ni mwendelezo katika siku zetu zote za maisha yetu,”alisisitiza Mtaturu.Mtaturu aliwatakia maandalizi mema ya sikukuu ya Eid El Fitri huku akiwaasa kusherehekea kwa amani,utulivu na upendo na kukumbuka kutoa Zaka kwa watu wasio na uwezo.

Alitumia nafasi hiyo kuwaomba wananchi kumuombea Rais Dokta John Magufuli kutokana na kazi kubwa anayoifanya katika kuendeleza dhamira yake ya kulinda rasilimali za nchi ili ziwanufaishe watanzania wote hasa wale wanyonge.

Kwa upande wake Sheikh wa wilaya hiyo Abdi Seleman akitoa neno la shukrani alimshukuru mkuu wa wilaya huyo kwa kuwafuturisha na kusema hiyo ni mara ya kwanza toka wilaya hiyo ianzishwe kwa mkuu wa wilaya kuwaalika futari.

“Kwa sadaka yako hii kwetu tunamuomba Mwenyezi Mungu akulipe kila la kheri,na inshallah huu usiwe mwisho bali uwe mwanzo wa kufanya hivi,”alisema Sheikh Seleman.

Nae Kadhi wa mkoa wa Singida Ramadhan Kaoja alimshukuru mkuu wa wilaya huyo na kusema hiyo ni dalili za kiongozi bora kwa kuwa karibu na jamii lakini pia ni sehemu ya kukamilisha imani yake ambapo kwa mwezi huu wa Ramadhan kwa kufuturisha anapata thawabu nyingi sana.


Hivyo makala DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA

yaani makala yote DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/dc-mtaturu-awaasa-waislamu-kuendeleza.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "DC MTATURU AWAASA WAISLAMU KUENDELEZA TABIA NJEMA"

Post a Comment