title : Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa
kiungo : Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa
Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa
MSHINDI wa Milioni 20 wa bahati nasibu ya Biko ‘Ijue Nguvu ya Buku’ wa droo ya 13, Amani Kabuku, jana amekabidhiwa fedha zake huku akisema kuwa zawadi hiyo ya donge nono itamkomboa kiuchumi, licha ya umri mdogo aliokuwa nao, akiwa na miaka 23 tu.
Makabidhiano hayo ya Biko na Kabuku ambaye pia anatokea katika familia ya mwanahabari nguri nchini Tanzania, Generali Ulimwengu, yalifanyika katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam, sambamba na kumpatia elimu ya kifedha saa chache kabla ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuingiza fedha zake alizoshinda katika droo hiyo ya aina yake.
Makabidhiano hayo ya Biko na Kabuku ambaye pia anatokea katika familia ya mwanahabari nguri nchini Tanzania, Generali Ulimwengu, yalifanyika katika benki ya NMB jijini Dar es Salaam, sambamba na kumpatia elimu ya kifedha saa chache kabla ya kufungua akaunti kwa ajili ya kuingiza fedha zake alizoshinda katika droo hiyo ya aina yake.
Alisema amecheza mara nne tu kabla ya kutangazwa mshindi katika droo ya 13 iliyofanyika Jumapili iliyopita, ambapo hata hivyo hakuamini haraka hadi alipowaona baadhi ya wafanyakazi wa Biko walipomfuata nyumbani kwao kwa ajili ya kumhakikishia juu ya ushindi huo.
“Ni furaha kubwa niliyokuwa nayo kwa sababu naamini huu ni wakati wa kuaga umasikini maana wengi wanatafuta nafasi kama hii ambayo leo Mungu ameniletea mimi ili niweze kutimiza ndoto zangu katika umri niliokuwa nao, hivyo nawashukuru Biko, huku nikiwataka Watanzania wacheze kwa wingi ili nao washinde kama ilivyokuwa mimi,”
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa Bahati Nasibu ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, akiwa katika furaha baada ya kukabidhiwa fedha zake katika benki ya NMB, jijini Dar es Salaam jana.
Mshindi wa Sh Milioni 20 wa droo ya 13 ya Biko 'Ijue Nguvu ya Buku', Amani Kabuku, katikati akiwa amepakatia fedha zake baada ya kukabidhiwa jijini Dar es Salaam jana. Kulia ni Meneja Masoko wa Biko, Goodhope Heaven na kushoto ni afisa wa NMB aliyekamilisha mchakato wa kufungua akaunti ya mshindi huyo na kuingiza pesa zake.
Akizungumza kwa furaha kubwa, mshindi huyo alisema ndio kwanza amemaliza kidato cha sita na kuibukia kwenye fedha hizo za Biko, hivyo anaamini zitamkomboa kiuchumi kwa ajili ya kuhakikisha kwamba maisha yake yanakuwa mazuri.
Hivyo makala Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa
yaani makala yote Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/06/amani-milioni-20-za-bahati-nasibu-ya.html
0 Response to "Amani: Milioni 20 za bahati nasibu ya Biko zitanikomboa"
Post a Comment