title : WADAU WA MAENDELEO WAMETAKIWA KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI YA KILL CHALLANGE
kiungo : WADAU WA MAENDELEO WAMETAKIWA KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI YA KILL CHALLANGE
WADAU WA MAENDELEO WAMETAKIWA KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI YA KILL CHALLANGE
Mwambawahabari
Na Mtumwa Ally
KAMPUNI ya Mgodi wa dhahabu Geita (GGM) kwa kushirikiana na Tume ya kupambana na maambuki ya Ukimwi nchini (TACAIDS) imewataka wadau mbali mbali wa maendeleo nchini kushiriki katika kampeni ya kill challange ili kuunga mkono jitihada za Serikali katika kupambana na maambukizi ya Ukimwi.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam jana Meneja Mawasiliano na Uhusiano wa mgodi huo,Tenga .B.Tenga alisema kuwa lengo la kampeni hiyo ni kusaidia jamii ambayo imeathirika na janga hilo.
Tenga alisema kuwa, kampuni hiyo imejenga vituo mbali mbali vya kutolea huduma ya upimaji pamoja kutoa ushauri nasaha kwa watu mbali mbali ambao wanafika katika vituo hivyo jambo ambalo linawapa faraja kwa kiasi kikubwa.
Alisema kuwa,tatizo la maambukizi ya virusi vya ukimwi ifike mahala watu wawe msatari wa mbele katika kutoa ushiriki wao wa hali na mali ili kuweza kukijenga kizazi kijacho kutokana na ongezeko la maambukizi ya ukwimwi.
"Tumefungua vituo vingi nchini ikiwemo kituo cha kulelea watoto yatima zaidi ya 100 ambao wameachwa na wazazi wao ambao wamefariki kwa maambukizi ya Ukimwi ambapo kila mwaka mfuko hutoa shilling million 150 kila mwaka ili kuweza kuwasaidia watoto hawa kwa mahitaji mbali mbali ambayo wanaweza kujiona kama na wao ni sehem ya jamii.
Tenga alisema kuwa zaidi ya Ngo's 40 zimenufaika na kampuni hiyo ambapo pia wamefanikiwa kujenga vituo mbali mbali ikiwemo Tanga,Shinyanga,Dodoma pamoja na Geita yenyewe ambako ndiko kwenye mgodi wenyewe jambo ambalo limetupa faraja kuona wanafika watu wengi zaid ukilinganisha kuna hospitali ya mkoa "alisema Tenga.
Aidha aliongeza kuwa, kutokana na changamoto kubwa walioipata mwaka jana kwa kupandisha watu wengi ambapo walikua na speed tofauti za kutembea ndio maana mwaka huu tumeamua kupandisha watu kidogo sana ili kuondoa usumbufu .
"Kwa mara hii watu watakao panda mlima watakua 40 na watakao endesha baskeli watakua 35 lengo ni kupata watu wenye nguvu moja kutokana na msafara huu kuongozwa na mtu mmoja" alisema Tenga.
Aliongeza kuwa,zoezi la upandaji mlima litachukua siku sita ambapo watapitia Machame na siku ya saba kushuka kwa kupitia njia ya Mweka lengo ikiwa ni kulinganisha maumivu wanayoyapata wapanda mlima ndio ambayo wanayapata wale walioathirika na virusi vya ukimwi.
Hivyo makala WADAU WA MAENDELEO WAMETAKIWA KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI YA KILL CHALLANGE
yaani makala yote WADAU WA MAENDELEO WAMETAKIWA KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI YA KILL CHALLANGE Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WADAU WA MAENDELEO WAMETAKIWA KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI YA KILL CHALLANGE mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/wadau-wa-maendeleo-wametakiwa-kushiriki.html
0 Response to "WADAU WA MAENDELEO WAMETAKIWA KUSHIRIKI KWENYE KAMPENI YA KILL CHALLANGE"
Post a Comment