TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018 - Hallo rafiki
WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts
makala afya,
makala biashara,
makala general,
makala hobby,
makala karibuni info,
makala michezo,
makala siasa,
makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.
title :
TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018kiungo :
TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018
TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018
Ofisa Programu wa Mtandao wa Jinsia Tanzania (TGNP), Alphonce Slima, akiongoza semina ya kujadili vipaumbele katika bajeti ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha wa 2017/2018 iliyofanyika makao makuu ya TGNP Mabibo jijini Dar es Salaam jana.
Mdau Neofita Kunambi akizungumza wakati akichangia mada kwenye semina hiyo.
Anna Sangai akichangia jambo kwenye semina hiyo.
Sadick Juma mkazi wa Mbezi Beach, akielezea changamoto ya upatikanaji wa dawa na vifaa tiba katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili.
Janeth Mawinza akielezea changamoto ya matibabu ya homa ya ini ambayo dawa zake hazipatikani nchini hadi zitoke India.
Moses Benard akizungumzia wajawazito kujinunulia vifaa vya kujifungulia na suala la dawati la ukatili wa kijinsia kuwepo vituo vya polisi.
Mdau Dalia Kalungwana akichangia jambo.
Washiriki wakiwa kwenye semina hiyo.
Semina ikiendelea.
wananchi wakifuatilia kwa karibu semina hiyo.
Vijana wakifuatilia mada katika semina hiyo.
WANANCHI wameiptia bajeti ya mwaka 2017/ 2018 ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia,Wazee na Watoto iliyotengwa na kuomba iongezwe kwa kuzingatia ukubwa wa wizara hiyo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti katika semina ya siku moja iliyoandaliwa na Mtandao wa Kijinsia Tanzania (TGNP) ya majadiliano ya kupitia bajeti hiyo ili kuona vipau mbele vyake waliombwa iongezwe ili iweze kukabiliana na changamoto zilizopo kwenye wizara hiyo ambayo imelemewa kutokana na ukubwa wake.
Kwa mwaka wa fedha wa 2016/ 2017 wizara hiyo ilitengewa bajeti ya sh.bilioni 845 ikilinganishwa na mwaka wa fedha wa 2017/2018 ambayo tofauti yake sio kubwa.
Akizungumza katika semina hiyo, Neofita Kunambi alisema katika wizara hiyo kunachangamoto kubwa bila ya kuongezewa fedha katika bajeti yake hazitaweza kuisha.
"Bila ya kuongeza bajeti katika wizara hii wajawazito wataendelea kujinunulia vifaa vya kujifungulia tunaomba jambo liangaliwe kwa karibu" alisema Kunambi.
Anna Sangai alisema huduma za afya zinapaswa kuboreshwa kuanzia upatikanaji wa dawa na vifaa tiba na bila kuongezwa kwa bajeti katika wizara hiyo itakuwa ni ndoto.
Mkazi wa Mbezi Beach, Sadick Juma alisema upatikanaji wa dawa, vifaa tiba, miundombinu na ukatili wa kijinsia ni changamoto kubwa katika wizara hiyo.
Alisema licha ya kuwepo duka la Bohari ya Dawa (MSD) katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili (MNH), upatikanaji wa dawa umekuwa mgumu hivyo kuifanya Muhimbili kuwa na majengo mazuri bila ya kuwa na dawa.
"Ukitaka kuona changamoto hata ukiwa ni mwanachama wa mfuko wa taifa wa bima ya afya (NHIF) ugua au uwe na mgonjwa ambaye ni mwanachama uende katika hospitali hiyo kwanza kupokelewa tu pale mapokezi ni balaa na ukifika muda wa kutakiwa kupata dawa utaambulia panado na kuambiwa dawa hazipo" alisema Juma.
Juma aliongeza kuwa huduma ya bure kwa watu wenye msamaha hiyo ni ndoto kwani wagonjwa hao hawasikilizwi kabisa jambo ambalo ni hatari.
Alisema serikali imekuwa ikijipodoa kuwa inaboresha huduma za afya lakini hali halisi haipo hivyo akitolea mfano kwa nchi nzima maduka ya dawa ya MSD yapo nane tu je upatikanaji wa dawa na vifaa tiba utafikia katika kiwango cha kukidhi mahitaji alihoji Juma.
Janeth Mawinza alisema bajeti hiyo iangalie zaidi jinsi ya kutibu magonjwa kama ya homa ya ini ambayo matibabu yake kwa hapa nchini hayapatikani mpaka dawa itoke nchini India.
Moses Benard alisema ikiwa mjamzito aliopo mjini anatakiwa kujinunulia vifaa vya kujifungulia hali ikoje kwa yule ambaye yupo kijijjini ambaye anachangamoto ya kutokuwa na fedha na kukimbiwa na mwenza wake hivyo akaomba Waziri wa wizara hiyo kutoa tamko rasmi la kuwataka wajawazito kutonunua vifaa hivyo wanapokwenda hospitali kujifungua.
Wadau wengine waliongelea jijini Dar es Salaam maeneo mengine kama Kipunguni wilayani Ilala kukosa kuwa na zahanati au hospitali hivyo kulazimika kwenda wilaya ya Kisarawe kupata matibabu jambo ambali linashangaza hivyo wakaomba bajeti ya wizara hiyo iongezwe ili kufanikisha upatikanaji wa zahanati au hospitali katika maeneo yao.
Hivyo makala TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018
yaani makala yote TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/tgnp-yaendesha-semina-kujadili.html
Related Posts :
Innocent Nyeriga: Milioni 20 za Biko nitajengea nyumbaKUTOKANA na changamoto nyingi za ukosefu wa makazi ya kuaminika kwa watu wengi, mshindi wa Sh Milioni 20, Innocent Nyeriga, amesema anatafak… Read More...
MASHINDANO YA MAGARI YAHITIMISHWA WILAYANI BAGAMOYO
… Read More...
Habari : Pitia Hapa Vichwa vya Habari vya Magazeti ya Leo, 08:08:2017
Wazalendo 25 Blog , is a Social Media which gives our Audience current News, Entertainment and Ad… Read More...
Matukio : Spika Mstaafu Anna Makinda atembelea banda la Benki ya DCB katika maonyesho ya nane nane Dodoma Spika Mstaafu Anna Makinda ameipongeza DCB Commercial Bank kwa huduma bora za kibenki inayotoa hasa huduma za mikopo kwa wajasirimali wadogo wadogo na kuwakwamua katika hali ya umasikini. Makinda amewaasa DCB Commercial Bank kujikita zaidi kutoa huduma hii kwa wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambao ndiyo wengi nchini ili kuboresha hali za maisha yao kwa kuwapatia mikopo. Hayo aliyasema wakati alipotembelea banda la DCB Commercial bank katika maonesho ya nane nane kanda ya kati yanayoendelea mkoani Dodoma. Makinda aliongezea kuwa ili kuwezesha wajasiriamali wengi DCB Benki haina budi kupeleka huduma hii ya mikopo nafuu kwa wajasiriamali wadogo wadogo vijijini ambako kuna uhitaji mkubwa wa huduma hii ya mikopo ya vikundi Sambamba na utoaji wa mikopo hii ya vikundi kwa wajasiriamali wadogo wadogo. Makinda ameasa DCB kuwaunganisha wajasiriamali hawa na huduma ya bima ya afya kutoka NHIF na pia bima ya taifa ya Jamii ili wateja hawa au familia zao wanapougua wapate msaada wa matibabu kwa unafuu hivyo kuwafanya wawe na afya na kuweza kurejesha mikopo . Alisisituza kuwa mteja akiugua ile pesa ya marejesho ataitumia katika kugharamia matibabu hivyo kuitia hasara benki, kumbe akijiunga na mifuko ya afya ya jamii atapata matibabu bure hivyo benki haitaathirika. Alisema makinda. Akimkaribisha kwenye banda na kuelezea huduma zinazotolewa na DCB Commecral Bank, Meneja masoko wa DCB benki Boyd Mwaisame alitaja huduma za DCB zinazopatikana katika banda la benki hiyo viwanja vya maonesho nane nane Mzuguni Dodoma kuwa ni pamoja na kufungua akaunti za kuweka akiba kwa watu binafsi, akaunti za wanafunzi, akaunti za muda maalumu, akaunti za biashara na huduma za mikopo kwa wajasiriamali wadogo, wakati na wakubwa. Mteja akisha fungua akaunti ya akiba na biashara anunganishwa bure na huduma ya DCB Pesa, huduma mpya ya kufanya miamala ya benki kupitia simu ya mkononi, yaani kuweka na kutoa pesa na kulipia bili mbalimbali. Huduma hii si lazima mteja awe na akunti DCB, bali mtu yeyote mtaani anaweza kujiunga mradi tu awe na namba yoyote ya simu ya mkononi iliyosajiliwa na mojawapo ya kitambulisha cha mpiga kura, utaifa, udereva na paspoti. Huduma hii inapatikana kwa kupiga *150*85#. Pia Meneja masoko alimueleza Mh. Makinda kuwa huduma za DCB Commercial Bank mbali na Dar es Salaam kwa sasa pia zinapatikana mkoani Dodoma kupitia tawi lake lilifunguliwa hivi karibuni katika jengo la LAPF mtaa wa Makole na mikoa mbali mbali kupitia huduma ya uwakala wa benki yaani DCB Jirani. Naye afisa wa benki Cecilia Msikula akimuelezea Mh. Makinda huduma ya akiba ya watoto akaunti za watoto –Young saver account ambayo alivutiwa sana nayo hasa Meli ya mtoto, alisema kuwa DCB inatoa huduma hii bila makato ya mwezi ambapo mteja akisha fungua akaunti ya mtoto kwa shi. 5,000 tu anapewa Meli ya Mtoto/ kibubu bure kumjengea mtoto utamaduni wa kujiwekea akiba akiwa bado mdogo kwa ajili ya matumizi yake ya baadaye. Pesa ikisha jaa kwenye Meli ya mtoto yaani kibubu mzazi analeta benki kwa ajili ya kuziweka kwenye akaunti ya mtoto baada ya kuzihesabu. Katika msafara huo, Spika mstaafu Makinda aliongozana na viongozi mbalimbali akiwemo Mkuu wa Wilaya ya Mpwawa Mh. Jabir Shekimweri. Spika Mstaafu Anna Makinda akikaribishwa na Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma. Spika Mstaafu Anna Makinda akisoma moja ya kipeperushi cha benki ya DCB katika banda lao katika Maonesho ya Nane nane yanaoendelea Mkoa wa Dodoma. Wa kwanza kulia ni Mkuu wa Masoko wa benki ya kibiashara ya DCB Boyd Mwaisame Wananchi wakipatiwa huduma katika banda la benki ya DCB katika Maonesho ya Nane Nane yanayoendelea Mkoani Dodoma.
Spika Mstaafu Anna Makinda ameipongeza DCB Commercial Bank kwa huduma bora za kibenki inayotoa hasa huduma za mikopo kwa wajasirimali wadog… Read More...
COSTECH ILIVYOWANOA MAOFISA UGANI WA MKOA WA LINDI KATIKA MAONYESHO YA NANENANE
Na Dotto Mwaibale, Lindi
MAOFISA ugani mkoani Lindi wamesema wanashindwa kuwahudumia kikamilifu wakulima kutokana na kukosekana kwa usafir… Read More...
0 Response to "TGNP Yaendesha Semina Kujadili Vipaumbele Katika Bajeti ya Wizara ya Afya Mwaka 2017/2018"
Post a Comment