Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini

Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini
kiungo : Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini

soma pia


Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini

Mwambawahabari

DSC_0761
Na. Immaculate Makilika
Serikali imetoa  asilimia miamoja ya fedha za bajeti ya dawa kwa mwaka  2016/2017  kwa ajili ya manunuzi ya dawa ikiwa ni moja ya mikakati ya kuboresha sekta ya afya nchini.
Akizungumza katika mahojiano ya kipindi cha TUNATEKELEZA kinachoratibiwa na Idara ya Habari – MAELEZO na kurushwa  na kituo cha televisheni cha TBC, Mkurugenzi  Mkuu wa Bohari Kuu ya Dawa  Laurean Bwanakunu alisema kuwa serikali inawahakikishia  wananchi kuwa katika mwaka wa fedha 2016/2017 imetenga fedha za kutosha ili kuhakikisha kuwa dawa zinapatikana katika vituo vya kutolea huduma za afya.

“Ikiwa ni  asilimia  81 ya upatikanaji wa dawa  pamoja na vifaa tiba katika maeneo ya mjini na vijijini, ambapo Bohari Kuu ya Dawa inahudumia vituo 5642 nchi kote” alisema Bwanakunu.
Pia, Bwanakunu alibainisha kuwa  hivi sasa kumekuwepo na upatikanaji wa dawa muhimu 110 kati ya 135   katika vituo  mbalimbali  vinavyotoa huduma za huduma  za afya.
Katika kuboresha huduma za usambazaji wa dawa nchini , Bohari Kuu ya Dawa imefanikiwa kufungua maduka ya dawa 7 katika mikoa ya Dar es salaam, Arusha, Geita, Mbeya  na Lindi, ambapo  imeanza kusafirisha dawa kwa kutumia  ndege na treni ili kufikisha dawa kwa wakati katika vituo mbalimbali vya afya nchini.
Aidha,  Mikoa na Halmashauri  zimetakiwa  kuwasilisha  maombi yao ya  dawa kwa wakati ili kutatua changamoto ya upungufu wa dawa katika vituo vya kutolea huduma za afya.


Hivyo makala Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini

yaani makala yote Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/serikali-yatoa-fedha-100-kwa-ajili-ya_16.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "Serikali Yatoa Fedha 100% Kwa Ajili Ya Manunuzi Ya Dawa Nchini"

Post a Comment