title : Rais wa Zanzibar Mh. Dk. Shein apokelewa na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh
kiungo : Rais wa Zanzibar Mh. Dk. Shein apokelewa na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh
Rais wa Zanzibar Mh. Dk. Shein apokelewa na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh
MwambawahabarRAIS
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein
amefanya mazungumzo na Rais wa Jamhuri ya Djibouti Ismail Omar Guelleh
ambapo katika mazungumzo hayo viongozi hao wamekubaliana kuanzisha
uhusiano na ushirikiano kati ya pande mbili hizo hasa katika sekta za
maendeleo na uchumi.
Viongozi walifanya mazungumzo katika ukumbi
wa Ikulu ya Djibouti ambapo Rais Dk. Shein alitumia fursa hiyo kutoa
pongezi na shukurani kwa Rais Guelleh kwa mwaliko wake huo nchini mwake.
Katika mazungumzo hayo viongozi hao kwa kauli moja walieleza
haja ya kuanzisha uhusiano na ushirikiano katika sekta mbali mbali za
maendeleo na uchumi kwa manufaa ya pande mbili hizo.
Rais wa Djibouti Ismail Omar Guelleh kwa upande wake alimuhakikishia Dk. Shein
kuwa nchi yake iko tayari kushirikiana na Zanzibar katika kuimarisha
sekta za mawasiliano, utalii, uwekezaji pamoja na usafiri na
usafirishaji sambamba na utayari wa kujifunza mambo mbali mbali kutoka
Zanzibar ikiwemo sekta ya utalii.
Rais Guelleh, alieleza kuwa
nchi yake inathamini sana uhusiano na ushirikiano uliopo kati yake na Tanzania ambao una historia nzuri na kueleza kuwa Djibout iko tayari kujifunza mbinu zilizotumika na Zanzibar katika kuimarisha sekta ya utalii.
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akisalimiana na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh alipofika katika Ikulu ya Djbout leo akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake,Picha na Ikulu.07/05/2017
RAIS wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk.Ali Mohamed Shein akifuatana na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh alipofika katika Ikulu ya Djbout leo akiwa katika ziara ya kiserikali na ujumbe wake,Picha na Ikulu.07/05/2017
Hivyo makala Rais wa Zanzibar Mh. Dk. Shein apokelewa na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh
yaani makala yote Rais wa Zanzibar Mh. Dk. Shein apokelewa na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Rais wa Zanzibar Mh. Dk. Shein apokelewa na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/rais-wa-zanzibar-mh-dk-shein-apokelewa_8.html
0 Response to "Rais wa Zanzibar Mh. Dk. Shein apokelewa na Rais wa Djbout Mhe.Ismail Omar Guelleh"
Post a Comment