title : NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHI - LUKUVI
kiungo : NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHI - LUKUVI
NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHI - LUKUVI
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa nyumba ardhi na Maendeleo ya Makazi Mhe. William Lukuvi amesema ataendelea kuwachukulia hatua wale wote ambao watakwenda kinyume cha sheria katika umiliki wa ardhi hapa nchini.
Mhe. Lukuvi alitoa kauli hiyo mbele ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli alipokuwa akijibu hoja za baadhi ya wajumbe wakati wa mkutano wa Baraza la Taifa la Biashara ambao walizungumzia changamoto kadhaa katika sekta ya ardhi.
“Kuna tatizo sana katika umiliki wa ardhi yetu, hasa haya mashamba makubwa, maana kuna baadhi ya watu wamechukua mashamba makubwa na kwenda kukopa katika mabenki na ukija katika hayo mashamba hakuna ambacho kimewekwa shambani kulingana na mikopo yao.
"Hivyo sasa sitasita kumchukulia hatua mtu yoyote ambaye atakwenda kinyume na na sheria za ardhi kwa kumnyang’anya hati yake na kuirudisha serikalini” amesema Waziri Lukuvi. Mhe. Lukuvi.
Pia ameweka wazi kuwa yupo radhi kutoa ardhi yenye hati ndani ya siku moja kwa mtu yoyote anayetaka kuwekeza viwanda hapa nchini na sio wababaishaji ambao wamegeuza ardhi kama mtaji wa kununulia mabasi kwa kukopa kwenye mabenki.
Mhe. Lukuvi alimalizia kwa kusema kwa sasa wizara yake imeandaa vitabu ambavyo vinaonyesha watu wote wale ambao wanamiliki ardhi bila ya kufanya shughuli yoyote .
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi William Lukuvi akielezea jambo wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam.
Waziri wa Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi mhe. William Lukuvi akizungumza na Gavana wa Benki kuu ya Tanzania Profesa Beno Ndulu
wakati wa Mkutano wa 10 wa Baraza la Taifa la Biashara Tanzania (TBNC) ambao pia uliambatana na uzinduzi wa Baraza hilo Ikulu Jijini Dar es Salaam Jumamosi.
Hivyo makala NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHI - LUKUVI
yaani makala yote NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHI - LUKUVI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHI - LUKUVI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/nitaendelea-kuwachukulia-hatua-wale.html
0 Response to "NITAENDELEA KUWACHUKULIA HATUA WALE WOTE WATAKAO KIUKA SHERIA ZA ARDHI - LUKUVI"
Post a Comment