Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele

Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele
kiungo : Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele

soma pia


Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele

Na Profesa Mbele
Leo, mwanahabari na mwanaharakati maarufu Amy Goodman amehutubia chuoni Carleton hapa Northfield. Mada yake ilihusu "threats to freedom of the press and the importance of independent media," yaani mambo yanayotishia uhuru wa vyombo vya habari na umuhimu wa media zisizo chini ya mamlaka yoyote. Ninaamini tafsiri yangu inaweza kuboreshwa.

Amy Goodman ni maarufu kama mwendesha kipindi kiitwacho Democracy Now!, ambacho kinachambua masuala kwa mtazamo tofauti na ule wa watawala wakandamizi na propaganda zao za kurubuni watu na kuhalalisha hali iliyopo. Mtazamo wa Amy Goodman ni wa kichochezi kwa maslahi ya walalahoi, wavuja jasho, na wale wanaoonewa na kudhulumiwa. Ni mwana harakati ambaye hasiti kujitosa sehemu ambapo watu wanadhulumiwa ili kuwaunga mkono na kuwezesha sauti zao kusikika ulimwenguni.
Katika mhadhara wake wa leo, ameongelea zaidi hali ya Marekani, akiainisha madhaifu ya vyombo vya habari na media kwa ujumla. Alianza hotuba yake kwa kauli ya kusisimua na kufikirisha ya Thomas Jefferson, "were it left to me to decide whether we should have a government without newspapers or newspapers without a government, I should not hesitate a moment to prefer the latter," yaani "ingekuwa ni mamlaka yangu kuamua kama tuwe na serikali bila magazeti au magazeti bila serikali, nisingesita hata dakika moja kuchagua hilo la pili."

Baada ya hotuba yake, Amy alisaini nakala za kitabu chake, Democracy Now: Twenty Years of Covering the Movements Changing America. Wakati ananisainia, aliniuliza ninatoka wapi. Nilipomtajia Tanzania, alitabasamu, akasema "Julius Nyerere." Niliguswa, ingawa sikushangaa, kuwa Amy ni mmoja wa watu wa ughaibuni wanaomwenzi Mwalimu Nyerere. 


Hivyo makala Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele

yaani makala yote Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mwanahabari-amy-goodman-amehutubia-hapa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mwanahabari Amy Goodman Amehutubia Hapa Kwetu - Profesa Mbele"

Post a Comment