Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili

Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili
kiungo : Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili

soma pia


Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili

Mwambawahabari

Mbunge  wa Tarime Vijijini kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema), John Heche ameshindwa kuendelea kuhudhuria vikao vya Bunge vinavyoendelea mjini hapa, kutokana na matatizo ya kiafya na kulazimika kukimbizwa katika Hospitali ya Taifa ya Muhimbili (MNH) jijini Dar es Salaam.

Heche alipata tatizo la afya na kufikishwa katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Dodoma jana alfajiri. Kwa mujibu wa Kaimu Mganga Mfawidhi wa Hospitali hiyo, Dk Caroline Damian alikiri kuwa Heche, alipokewa hospitalini hapo alfajiri ya jana na kuhudumiwa kwa muda kabla hajasafirishwa kupelekwa mahali ambako hakuwa tayari kupataja.

“Hatujampa rufaa ila matibabu yake yanaratibiwa na Kliniki ya Bunge, hivyo tulimpokea na kumhudumia kwa muda kabla taratibu za kumsafirisha hazijakamilika, tulipoambiwa ndege ya kumsafirisha ipo tayari, aliondolewa kwetu na kusafirishwa kwa ajili ya matibabu,”alieleza daktari huyo.

Awali, mbunge huyo alipata tatizo la afya na kulazimika kuwa chini ya uangalizi wa kitabibu. Awali, Naibu Katibu Mkuu wa Chadema Zanzibar, Salum Mwalimu, alikaririwa na vyombo vya habari hivi karibuni akijibu maswali ya wananchi walihoji hali ya mbunge huyo, ambaye ilikuwa ikielezwa kuwa hospitalini.

Kabla ya muda huo kuwadia, ilielezwa kuwa Heche alipata maumivu ya tumbo kabla hajapelekwa katika Hospitali ya Rufaa ya Taifa ya Muhimbili ambako alifanyiwa upasuaji. 

Kwa upande wake, Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano wa Chadema Taifa, Tumaini Makene jana  alithibitisha taarifa ya kuugua ghafla kwa Heche na kuletwa jijini Dar es Salaam katika hospitali hiyo.

“Ni kweli Heche aliugua ghafla akiwa Bungeni huko Dodoma, alisafirishwa kwa ndege jana asubuhi saa moja na kuletwa Muhimbili ambako anaendelea na matibabu,” alisema Makene.

Ofisa Habari wa Muhimbili, Neema Mwangomo alithibitisha kupokelewa Heche jana saa nne asubuhi na kwamba anaendelea na vipimo kubaini nini tatizo lake.


Hivyo makala Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili

yaani makala yote Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/05/mbunge-john-heche-azidiwa-ghafla-na.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "Mbunge John Heche Azidiwa Ghafla na Kukimbizwa Muhimbili"

Post a Comment