title : TFF LAWAMANI, HAWAPOKEI SIMU ZA THE MIGHTY ELEPHANT FC
kiungo : TFF LAWAMANI, HAWAPOKEI SIMU ZA THE MIGHTY ELEPHANT FC
TFF LAWAMANI, HAWAPOKEI SIMU ZA THE MIGHTY ELEPHANT FC
Na Alex Mapunda, Ruvuma
KATIBU wa timu ya Daraja la Pili, The Mighty Elephant Fc toka Songea Rajabu Dau, amesikitishwa na viongozi wa Shirikisho la soka hapa nchini TFF kwa kushindwa kupokea simu yake zaidi ya mara nne pindi anapowapigia ili kuulizia kuhusu Rufaa yao kuhusu upangwaji wa Matokeo kati ya Timu ya Mawenzi dhidi ya Saba Saba zote za Morogoro.
Dau amesema kila akiwapigia simu TFF simu zao zinaita bila Majibu, suala ambalo linaleta mashaka kwa kuwa rufaa yao toka walipopeleka ina takribani miezi Miwili na TFF wako kimya hadi leo wakati wao walifuata Taratibu zote za kukata rufaa zilizowekwa na TFF.
“TFF wanatukosea, napiga simu ya Katibu Mkuu wa TFF Selestine Mwesigwa hapokei, Eliud Mvela naye hapokei simu. Kwanini wanakaa Kimya wakati Rufaa walishapokea na uthibitisho walishanipa?
Mbona rufaa za timu kubwa wanazifanyia maamuzi mapema? Au sisi kwa kuwa tupo ligi daraja la pili hatuna haki?, TFF naomba watume majibu ya rufaa yetu, kabla hatujafanya maamuzi magumu. ”
“Sisi tulikata rufaa kuhusu kupinga matokeo ya Sabasaba na Mawenzi, matokeo ambayo yalipangwa na chama cha soka mkoa wa Morogoro ili kuipandisha timu moja kwa nguvu.
Tuna sauti ya dakika 23 ya kikao cha siri ambacho kiliwakutanisha viongozi wa soka Morogoro, viongozi wa SabaSaba pamoja na Mawezi ambapo wote walikubaliana Sabasaba acheze chini ya kiwango ili Mawenzi apate pointi tatu kitu ambacho ni kinyume cha sheria na taratibu za mpira wa miguu”
“ Lakini baada ya Mawenzi kupata pointi Tatu toka kwa Sabasaba, kwenye kikao hicho Mwenyekiti wa Chama cha Soka Morogoro aliahidi kuisaidia Saba Saba isishuke daraja kwa kutumia fedha. Katika kikao hicho walikuwepo hadi viongozi wa Serikali na sauti zao zimesikika” alisisitiza Dau.
Lakini taarifa toka kijiweni kwa wadau wa soka wao wanasema TFF wanashindwa kutolea uamuzi kuhusu suala la The Mighty Elephnt Fc kwa kuwa Uchaguzi umekaribia na Chama cha Soka cha Morogoro ni moja ya Kambi muhimu upande wa Malinzi.
Timu ya Mawenzi, Sabasaba na The Mighty Elephant wote walikuwa kundi moja katika ligi daraja la pili ambayo imemalizika hivi karibuni.
Hivyo makala TFF LAWAMANI, HAWAPOKEI SIMU ZA THE MIGHTY ELEPHANT FC
yaani makala yote TFF LAWAMANI, HAWAPOKEI SIMU ZA THE MIGHTY ELEPHANT FC Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TFF LAWAMANI, HAWAPOKEI SIMU ZA THE MIGHTY ELEPHANT FC mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/tff-lawamani-hawapokei-simu-za-mighty.html
0 Response to "TFF LAWAMANI, HAWAPOKEI SIMU ZA THE MIGHTY ELEPHANT FC"
Post a Comment