title : MAAJABU ALLY MADIWA: MTEULE WA EJAT 2016 PEKEE KUTOKA TANGA
kiungo : MAAJABU ALLY MADIWA: MTEULE WA EJAT 2016 PEKEE KUTOKA TANGA
MAAJABU ALLY MADIWA: MTEULE WA EJAT 2016 PEKEE KUTOKA TANGA
Na Mohammed Hammie Rajab
"Hujambo msikilizaji wa Pangani Fm na karibu katika kipindi cha Sauti Ya Mwanamke, kipindi hiki ni mahsusi kwa ajili ya kujadili changamoto mbali mbali anazokabiliana nazo mwanamke...." Ni sauti yake Maajabu Ally Madiwa anapokuwa redioni akitangaza kipindi.
Sauti yake iliyojaa bashasha ya kumfanya kila msikilazaji wa redio Pangani Fm iliyopo wilayani Pangani mkoani tanga atake kuisikia awapo redioni ndiyo iliyomfanya mpaka sasa awe miongoni mwa waandishi wa habari wadogo Tanzania wenye vipaji vya hali ya juu.
Uwezo wake wake kutangaza na kutambua aina gani ya habari inapaswa kutolewa kwa jamii anayoifanyia kazi uligunduliwa na shirika la Uzikwasa lenye kufanya
shughuli zake wilayani Pangani, ambalo linaelimisha jamii kwa kutimia sanaa.
Shirika hili limekuwa msaada mkubwa katika kuelimisha jamii ya Pangani kuachana na tabia hatarishi, kupinga ukatili dhidi ya watoto, wasichana na wanawake, na kuhakikisha viongozi
wanatekeleza majukumu yao kwa mguso.
Huko ndipo ambapo Maajabu Ally Madiwa aliponogesha uwezo wake mpaka kuwa miongoni mwa wateule 66 wa Tuzo za Umahiri wa Uandishi wa Habari Tanzania (EJAT) kwa mwaka 2016 kati ya washindani 810.
Hivyo makala MAAJABU ALLY MADIWA: MTEULE WA EJAT 2016 PEKEE KUTOKA TANGA
yaani makala yote MAAJABU ALLY MADIWA: MTEULE WA EJAT 2016 PEKEE KUTOKA TANGA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MAAJABU ALLY MADIWA: MTEULE WA EJAT 2016 PEKEE KUTOKA TANGA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/maajabu-ally-madiwa-mteule-wa-ejat-2016.html
0 Response to "MAAJABU ALLY MADIWA: MTEULE WA EJAT 2016 PEKEE KUTOKA TANGA"
Post a Comment