title : KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII
kiungo : KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII
KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII
Baraza la Wafanyakazi linaundwa kwa mujibu wa matakwa ya kisheria ya uwepo wa Baraza la Wafanyakazi mahali pa kazi ambalo linaendesha shughuli zake kwa kuzingatia Mkataba wa Baraza la wafanyakazi.
Kwa kutambua hilo, Naibu Waziri wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Jinsia,Jinsia Wazee na Watoto, Mhe. Dkt. Hamis A. Kingwangala amefungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi wa Idara Kuu ya Maendeleo ya Jamii uliofanyika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo Kukuu cha Dodoma kwa ili kujadili na kutoa maoni kuhusu utekelezaji wa majukumu ya wizara kwa mwaka 2016/17 na mpango na bajeti ya wizara 2017/18.
Akifungua mkutano huo, Mgeni rasimi Mhe. Kigwangalla alipongeza viongozi wa TUGHE kuanzia ngazi ya Tawi hadi Taifa kwa kudumisha mahusiano rafiki mahala pa kazi, na kuweza kutoa ushauri ambao umesaidia kuaminiana na kuimarisha mahusiano baina ya menejimenti na wafanyakazi wa Wizara.
Mhe. Naibu Waziri ametoa rai kuwa, ili kufikia dira, dhima na malengo ya Wizara tunahitaji kuwa na mpango na bajeti inayozingatia utekelezaji wa vipaumbele vilivyowekwa. Kwa kutambua hilo Bajeti ya Idara kuu ya Maendeleo ya Jamii imeaandaliwa kwa muktadha huo, na pia inaakisi sera, mipango, mikakati ya Taifa, Ilani ya Uchaguzi ya Chama Tawala na mikataba ya Kikanda na Kimataifa.
Katika kufanikisha malengo hayo ya Mhe. Naibu Waziri amesisitiza kila mtumishi kufanya kazi kwa bidii na maarifa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Na pia Wizara amesisitizwa kuendelea kutoa motisha kwa watumishi wanaowajibika, wabunifu na wenye maadili mema ili kuwa kichocheo cha ubunifu, tija na ufanisi sehemu ya kazi.
Naibu Waziri ameipongeza Wizara kwa kufanikiwa kuandaa Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi na kuwataka kutumia weledi na umahiri wa watumishi kukabiliana na changamoto zilizopo na kufanikisha utekelezaji wa majukumu ya Wizara ambayo ni pamoja na kuelimisha jamii kuondokana na mila na desturi zenye madhara kama ukeketaji ambao sasa tuna asilimia 10 na ndoa za utotoni asilimia 37; kuamsha ari ya jamii kushiriki katika shughuli za maendeleo na ustawi wao; kufanya ufuatiliaji wa mashirika Yasiyo ya Kiserikali ili kuhakikisha wanazingatia sheria, kanuni na taratibu. Aidha, ameelekeza Wizara kusimamia utekelezaji wa Mpango wa Kitaifa wa Kudhibiti Vitendo vya Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto ambao tumejipangia kupunguza ukatili kwa asilimia 50 ifikapo mwaka 2025.
Mhe. Kigwangala amebainisha mambo manane ambayo Wizara inatakiwa kuyazingatia. Mambo hayo ni kutimiza haki na wajibu kwa kila mtumishi kutoa mchango wa mawazo na ushauri kwenye utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2016/17 na Mpango na Bajeti ya mwaka 2017/18. Pili, kushiriki kujadili changamoto za kiutekelezaji na kuzibadili kuwa fursa kwa kutoa ushauri na mapendekezo ya namna ya kuboresha utendaji. Tatu, kutekeleza majukumu kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu za utumishi wa umma. Nne, kuitikia utekelezaji wa Mpango wa Taifa wa Kutokomeza Ukatili dhidi ya Wanawake na Watoto kusimamiwa ipasavyo na shirikishwa wa wadau wote.
Maeneo mengine ni kuhakikisha kuwa Wataalam wa wizara wanashirikiana na OR TAMISEMI ili kuhuisha ari ya wananchi kushiriki shughuli za maendeleo yao. Sita, kuimarisha mahusiano na OR TAMISEMI ili kuhakisha wataalam waliopo kwenye ngazi za Mikoa na Halmashauri wanatumika na kutekeleza majukumu ipasavyo. Saba, Vyuo vya maendeleo ya jamii kutoa elimu inayoandaa wataalam wenye weledi na mahiri katika kutekeleza kazi za maendeleo ya jamii. Mwisho, Watumishi kuwa na hadhari na tabia hatarishi zinazopelekea maambukizi ya ukimwi na kwa upande mwingine mwajiri aendelee kutoa huduma kwa wathirika kwa mujibu wa bajeti.
Mapema akimkaribisha Mgeni Rasmi, Katibu Mkuu wa Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia Wazee na Watoto, Bibi Sihaba Nkinga alimfahamisha Mgeni Rasimi kuwa, wajumbe wa Baraza la Wafanyakazi watajadili Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa Fedha 2017/18. Kwa mujibu wa Sheria inayounda mabaraza ya wafanyakazi mahali pa kazi kwani ni lazima Bajeti ya Wizara ipitishwe na Baraza la Wafanyakazi. Agenda ya pili, ilikuwa kupitia na kufanyia marekebisho muundo wa Baraza ili kujumuisha Idara ya Ustawi wa Jamii, iliyounganishwa kutoka Idara Kuu ya Afya, baada ya mabadiliko ya muundo wa Wizara. Aidha, baada ya Vyuo vya Maendeleo ya Wananchi kuhamia Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia Wizara imeona kuna umuhimu wa kuwa na wawakilishi wa Vyuo vya Maendeleo ya Jamii na Ustawi wa Jamii kwa uwakilishi wa menejimenti na uwakilishi wa watumishi.
Katibu Mkuu Sihaba, alifafanua tunu za Wizara kwamba, ari waliyonayo watumishi katika kutimiza majukumu yao kwa weledi, uadilifu, juhudi na maarifa katika kuchangia maendeleo na ustawi endelevu wa Taifa. “Katika hili tumeendelea kuhamasisha jamii na kutoa elimu kuhusu maendeleo na ustawi wa jamii, usawa wa kijinsia, uratibu wa mashirika yasiyo ya kiserikali na maendeleo ya mtoto kwa jamii, maafisa wa serikali na wadau wengine wa maendeleo”. alisema.
Kitengo cha Mawsiliano Serikalini
Wizara ya Afya, Mendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto
Idara Kuu ya Mendeleo ya JamiiHivyo makala KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII
yaani makala yote KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2017/04/kigwangalla-afungua-mkutano-wa-baraza.html
0 Response to "KIGWANGALLA AFUNGUA MKUTANO WA BARAZA LA WAFANYAKAZI IDARA KUU YA MAENDELEO YA JAMII"
Post a Comment