title : MCHUNGAJI MASHIMO ATOA MAONO MAZITO.
kiungo : MCHUNGAJI MASHIMO ATOA MAONO MAZITO.
MCHUNGAJI MASHIMO ATOA MAONO MAZITO.
Mchungaji wa Mitume, Manabii na Maaskofu Tanzania Commando Mashimo akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Viongozi wa serikali wametakiwa kuwa na hofu ya mungu katika utekelezaji wa majukumu yao ikiwemo kutenda haki katika kufanya maamuzi .
Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam Mchungaji wa Mitume, Manabii na Maaskofu Tanzania Commando Mashimo, amesema kuwa kupitia maombi yake mwenyezi mungu amemuonesheya maono kuna mtumishi wa umma anaitesa familia fulani ambayo ipo mkoa wa kusini.
Mchungaji Mashimo amesema kuwa maono hayo yameonesha mtumishi mmoja wa umma jinsi anavyoitesa familia hiyo kwa kutumia madaraka yeke jambo ambalo sio rafiki mbele za mungu.
"Naomba mtumishi huyo akatubu katika familia hiyo, tofauti na hapo anaweza kufariki dunia au kupata aibu kutokana na mambo anayofanya" amesema Mchungaji Mashimo.
Hata hivyo mchungaji huyo akubainisha jina la mtumishi huyo wa umma pamoja na familia inayoteswa kwa kile kinachokidai katika maono yake mwenyezi mungu akumuonesha jina pamoja na ukoo wa hiyo familia.
Katika hatua nyengine mchungaji Mashimo amesema kuwa wakati umefika viongozi wa serikali katika ngazi mbalimbali kufanya kazi zao kwa kutenda haki jambo ambalo litasaidia kuunga mkono juhudi za Rais Dkt. John Pombe Magufuli.
"Ni jambo jema viongozi wa umma kutenda haki katika majukumu yao, kitu ambacho itasaidia kuleta maendeleo" amesema Mchungaji Mashimo.
Hivyo makala MCHUNGAJI MASHIMO ATOA MAONO MAZITO.
yaani makala yote MCHUNGAJI MASHIMO ATOA MAONO MAZITO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MCHUNGAJI MASHIMO ATOA MAONO MAZITO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/mchungaji-mashimo-atoa-maono-mazito.html
0 Response to "MCHUNGAJI MASHIMO ATOA MAONO MAZITO."
Post a Comment