title : DAR ES SALAAM YAMALIZA UGAWAJI VITAMBULISHO AWAMU YA KWANZA
kiungo : DAR ES SALAAM YAMALIZA UGAWAJI VITAMBULISHO AWAMU YA KWANZA
DAR ES SALAAM YAMALIZA UGAWAJI VITAMBULISHO AWAMU YA KWANZA
Mkoa wa Dar es Salaam umekuwa kinara wa kutimiza agizo la Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe.Dr. John Pombe Magufuli la kutoa vitambulisho bure kwa wafanyabiashara wadogo wadogo(maarufu wamachinga) kwa nia ya kurasimisha sekta hii Muhimu katika ujenzi wa Taifa.Zoezi hili la ugawaji wa vitambulisho 25,000 kwa awamu ya kwanza lilikamilika tangia tarehe 03/01/2019 na kuufanya Mkoa huu kuwa Mkoa wa kwanza kitaifa katika kukamilisha zoezi hili la ugawaji.
Kutokana na kukamilisha kwa haraka kwa zoezi hili Mkoa wa Dar es Salaam umepokea tayari vitambulisho vingine 25,000 kwa ajiri ya ugawaji wa awamu ya pili.
Akizungumza katika makabidhiano ya vitambulisho hivyo kwa wakuu wa wilaya wa Mkoa huu, Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam Mhe.Paul Makonda amemshukuru Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kukubali ombi la nyongeza ya vitambulisho vingine 25,000 kwa wafanyabiashara wa Mkoa wa Dar es Salam ambavyo vitaanza kugaiwa katika wilaya zote kuanzia kesho siku ya jumanne ya tarehe 08/01/2019.
Katika hatua nyingine Mhe. Makonda amesisitiza katika ufuatajwi wa sheria na kanuni katika ugawaji wa vitambulisho hivyo na kusisitiza kuwa vitambulisho hivyo haviuzwi Bali kiasi cha tshs 20,000 inayotolewa na wafanyabiashara wadogo ni mchango wa gharama za utengenezwaji na si vinginevyo, hivyo kukemea vikali ulanguzi wowote ambao unaweza kutokea katika zoezi hili la ugawaji.
Vitambulisho hivyo vimekabidhiwa kwa wakuu wa Wilaya wa Mkoa wa Dar es Salaam na kupokelewa kwa niaba Yao na Mkuu wa Wilaya ya Temeke Mhe,Felix Lyaniva.
Hivyo makala DAR ES SALAAM YAMALIZA UGAWAJI VITAMBULISHO AWAMU YA KWANZA
yaani makala yote DAR ES SALAAM YAMALIZA UGAWAJI VITAMBULISHO AWAMU YA KWANZA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala DAR ES SALAAM YAMALIZA UGAWAJI VITAMBULISHO AWAMU YA KWANZA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2019/01/dar-es-salaam-yamaliza-ugawaji.html
0 Response to "DAR ES SALAAM YAMALIZA UGAWAJI VITAMBULISHO AWAMU YA KWANZA"
Post a Comment