title : UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA JOHNS HOPKINS CHA MAREKANI WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR
kiungo : UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA JOHNS HOPKINS CHA MAREKANI WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR
UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA JOHNS HOPKINS CHA MAREKANI WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR
Waziri wa Afya Zanzibar Mhe.Hamad Rashid Mohamed akizungumza na ujumbe wa Madaktari kutoka Chuo Kikuu cha JOHNS HOPKINS cha Marekani ulipofika ofisi ya Wizara ya Afya Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar.
Ujumbe wa Madaktari kutoka Chuo Kikuu cha JOHNS HOPKINS uliofika Zanzibar kuja kuangalia miradi ya Malaria inayofadhiliwa na Marekani kwa upande wa Zanzibar.
Waziri wa Afya Zanzibar Hamad Rashid Mohamed akisalimiana na kiongozi wa msafara wa Madaktari kutoka Chuo Kikuu cha JOHNS HOPKINS Nchini Marekani Bi Ellen J MacKenzie alipofika ofisini kwake Mnazi Mmoja Mjini Zanzibar kwaajili ya kujitambulisha .
Mkurugenzi wa Chuo cha JOHNS HOPKINS cha Marekani kwa Tanzania Waziri Nyoni akizungumzi na Waandishi wa habari, hawapo pichani kuhusiana na ujumbe wa madaktari uliofika nchini kukagua miradi ya malaria kwa upande wa Zanzibar. Picha na Abdalla Omar-Maelezo Zanzibar.
Na Ali Issa –Maelezo Zanzibar 23/10/2018
Wizara ya Afya Zanzibar imesema kiwango cha ugonjwa wa Malaria kilichopo nchini kwa sasa kinaridhisha kutokana na juhudi mbalimbali zinazochukuliwa kuutokomeza ugonjwa huo nchini.
Ugonjwa huo kwa sasa upo chini ya asilimia moja na hivyo juhudi mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na Wadau tofauti ili kuutokomeza nchini.
Waziri wa Afya Hamad Rashid Mohamed ameyasema hayo alipokutana na ujumbe wa Madaktari 20 kutoka Chuo cha Udaktari cha Johns Hopkin Bloomberg cha Marekani huko Ofisini kwake Mnazi mmoja mjini Zanzibar.
Waziri Hamad amesema amefurahishwa na ujio huo kutoka Marekani uliokuja kukagua Miradi ya kupambana na ugonjwa wa Malaria inayofadhiliwa na Serikali ya Marekani.
Amesema kupitia ziara hiyo Wageni hao wataweza kufanya tathmini ya kiwango cha Malaria nchini na kuweza kujua mafanikio na changamoto zilizopo katika uendeshaji wa Mradi huo wa kupambana na Malaria.
Hata hivyo Waziri wa Afya aliwaelezea Wageni hao mafanikio yaliyopatikana ikiwa ni pamoja na kuubakisha ugonjwa huo chini ya asilimia moja nchini.
Waziri wa Afya ameendelea kutoa wito kwa wananchi
kuendelea kutumia Vyandarua vilivyotiwa Dawa na
kuyaweka mazingira safi ili kujikinga na Mbu wanaoweza
kueneza ugonjwa huo.
Amewashukuru Madaktari hao kwa juhudi wanazozichukuwa na kuwaomba kuzidisha mashirikiano kwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar ili wananchi wa chini waweze kufaidika.
Hata hivyo aliwaomba kufanya Tafiti nyengine za Maradhi mengine yasio ambukiza ili kuweza kuyatokomeza nchini.
Kwa upande wake Mkurugenzi wa cha JOHN HOPKINS nchini Tanzania Waziri Nyoni aliishukuru Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar kupitia Wizara ya Afya namna inavyopambana kuhakikisha ugonjwa huo unatokomezwa nchini.
Amesema mafanikio hayo pia yanatokana na juhudi zinazofanywa na Chuo cha JOHN HOPKINS kwa kushirikiana na Serikali na wadau mbalimbali ili kuhakikisha afya za Wananchi wa Zanzibar zinazidi kuimarika.
Aidha Mkurugenzi Nyoni amelipokea ombi la kufanya tafiti za maradhi mengine yasiyoambukiza ili wayafanyie kazi kulingana na hali zinavyoruhusu.
Hivyo makala UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA JOHNS HOPKINS CHA MAREKANI WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR
yaani makala yote UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA JOHNS HOPKINS CHA MAREKANI WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA JOHNS HOPKINS CHA MAREKANI WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/ujumbe-wa-madaktari-kutoka-chuo-kikuu.html
0 Response to "UJUMBE WA MADAKTARI KUTOKA CHUO KIKUU CHA JOHNS HOPKINS CHA MAREKANI WAKUTANA NA WAZIRI WA AFYA ZANZIBAR"
Post a Comment