TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI

TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI
kiungo : TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI

soma pia


TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI

Na Mwamvua Mwinyi, FUKAYOSI 
BAADHI ya wakulima kitongoji cha Segwa, kata ya Fukayosi Bagamoyo mkoani Pwani, kinakabiliwa na tatizo la uvamizi wa tembo ambao wameharibu mazao yao kwenye hekari kumi na kuvunja nyumba mbili. 

Akielezea kero hiyo wakati wa ziara ya mbunge wa jimbo la Bagamoyo, Dk.Shukuru Kawambwa, katika kata ya Fukayoso, mwenyekiti wa kijiji cha Mwavi,Shabani Mkumbi alisema ,tembo wamekuwa wakitokea hifadhi ya Taifa Saadani na kuvuka mto WAMI na kuingia katika maeneo ya watu kwenye vijiji vya Fukayosi  na Mwavi . 

"Mazao yaliyoharibiwa ni muhogo 
,matikiti,nyanya Maji ,nyanya chungu,maboga , hoho, mananasi, migomba na miwa ." alisema.
 
Mkazi wa Segwa Hassan Kalahuka alisema ,kutokana na tatizo hilo wameamua kuunda kamati ambayo itafuatilia suala la fidia kupitia ofisi ya wilaya kwani wao wamekwama. 

Mmoja wa aliyeathiriwa shamba lake na tembo hao ,Ramadhani Mfaume alielezea ,mbali ya kuharibiwa mazao yake pia gunia zake kumi zimeharibiwa. 

Alibainisha tangu apate hasara hiyo agost 21 mwaka huu hajalipwa kifuta jasho hadi sasa hivyo amemuomba mbunge Kawambwa kuwasaidia. 

Akipokea kero hiyo kubwa, Dk .Kawambwa alisema amepokea taarifa hiyo na ataangalia namna ya kuzungumza na TANAPA, wilaya na wizara husika kuona namna watakavyosaidiwa. 

Akiwa katika kitongoji hicho alifikishiwa bado kuna kero ya ukosefu wa maji safi na salama, wanatumia maji ya visima vya asili ambapo mvua zikikatika wanapata shida zaidi. 

Dk.Kawambwa aliwaambia serikali inaendelea kutatua tatizo la maji kwa kutekeleza miradi mbalimbali ikiwemo mradi wa CHALIWASA, ili hali kupunguza makali ya kero hiyo. 


Hivyo makala TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI

yaani makala yote TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tembo-waharibu-mazao-ya-wakulima-segwa.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "TEMBO WAHARIBU MAZAO YA WAKULIMA SEGWA HUKO FUKAYOSI"

Post a Comment