title : TANZANIA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI YA PAMOJA YA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
kiungo : TANZANIA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI YA PAMOJA YA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
TANZANIA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI YA PAMOJA YA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
Na Khadija seif, Globu ya jamii
NCHI ya Tanzania inatarajiwa kuwa mwenyeji wa mazoezi ya kijeshi ya pamoja kwa nchi za Jumuiya ya Afrika mashariki ambayo yatafanyika kuanzia Novemba 5 mpaka 21 mwaka huu mkoani Tanga.
Akizungumza leo jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Mafunzo na Operesheni ya kivita jeshini wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Meja Jenerali Alfred Kapinga ametaja baadhi ya nchi ambazo zitashiriki ni Burundi, Rwanda,Kenya,Uganda na Tanzania ambaye ndiye mwenyeji wa mafunzo hayo ambayo yatafanyika
wilayani Muheza mkoani Tanga. Mafunzo hayo yatafafahamika kwa jina la Ushirikiano Imara 2018.Pia amesema kwenye mafunzo hayo pamoja ni mambo mengine yatalenga kujenga uwezo wa kukabiliana na uhalifu pamoja na majanga huku akieleza namna ambavyo yatasaidia kubadilishana uzoefu wa kiutendaji, kuimarisha uhusiano baina ya nchi, majeshi ya Afrika Mashariki pamoja na taasisi zingine za kiraia ambazo
zitashiriki zoezi hilo.
Ameongeza katika kipindi hicho cha mafunzo kutakuwa na kazi za kusaidia jamii katika shughuli mbalimbali zikiwemo ujenzi wa madarasa, ofisi za walimu pamoja na vyoo katika Shule ya Msingi ya Machemba iliyopo wilayani Muheza mkoani Tanga, pia kutakuwa na utoaji wa huduma za tiba kwa wananchi katika eneo la zoezi.
Mkuu wa Mafunzo na Operesheni ya kivita jeshini wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Meja Jenerali Alfred Kapinga , akizungumza na Waandishi wa Habari juu ya Mazoezi ya Pamoja ya kijeshi yatakayofanyika Mkoani Tanga mwaka huu
Mkuu wa Mafunzo na Operesheni ya kivita jeshini wa Jeshi la Ulinzi la Wananchi wa Tanzania(JWTZ) Meja Jenerali Alfred Kapinga akiwa na Waandishi wa Habari
Hivyo makala TANZANIA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI YA PAMOJA YA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI
yaani makala yote TANZANIA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI YA PAMOJA YA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TANZANIA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI YA PAMOJA YA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/tanzania-mwenyeji-wa-mazoezi-ya-kijeshi.html
0 Response to "TANZANIA MWENYEJI WA MAZOEZI YA KIJESHI YA PAMOJA YA NCHI ZA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI"
Post a Comment