title : MSICHAGUE VIONGOZI MAZEZETA NA MANANGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019-SAMIA
kiungo : MSICHAGUE VIONGOZI MAZEZETA NA MANANGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019-SAMIA
MSICHAGUE VIONGOZI MAZEZETA NA MANANGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019-SAMIA
NA MWAMVUA MWINYI,KIBAHA
MAKAMU wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ,Samia Suluhu amewataka wananchi wa Kibaha Mjini Mkoani Pwani ,wajipange kuchagua viongozi wepesi kufuatilia maendeleo na kwenda mbio badala ya kuchagua mazezeta na mananga ,katika uchaguzi unaokuja wa serikali za mitaa- 2019.
Akihitimisha ziara yake ya siku sita mkoani hapo katika mkutano wa hadhara ,Mailmoja Samia aliwasihi wasichague watu wazito,wezi na mafisadi bali waweke viongozi watakaojenga Kibaha .
"Wanasema mjenga nchi ni mwananchi mwenyewe ,mimi nikija ninaona kasoro zilizopo nitakwambieni kuna kasoro lakini warekebishaji ni nyinyi na viongozi mtakaowachagua ""Mkichagua wazuri wataondosha kasoro zilizopo haraka lakini mkichagua wazito na mananga hapa yatazama tuu chini kunyanyuka hayanyanyuki ,kutembea hayatembei "alisisitiza Samia .Akizungumzia suala la ardhi anasema",Wakati napita ,mheshimiwa mkuu wa mkoa alinionyesha eneo kubwa halina kitu chochote nikamwambia mnataka manispaa ,lakini mbona eneo hili mwitu mtupu hakuna kuendelezwa akaniambia linamilikiwa na taasisi fulani "
Aidha ,ameitaka wilaya na halmashauri ya Mji huo kukaa chini na taasisi ambazo zimehodhi maeneo bila kuyaendeleza katika kipindi kirefu ili ziweze kuingia ubia .Awali Mbunge wa jimbo la Kibaha Mjini ,Silvestry Koka aliomba mji huo upandishwe hadhi na kuwa manispaa kama vigezo vinaruhusu.Alitaja changamoto zinazowakabili kuwa ni ,usambazaji wa maji kwenda kwa wananchi unasuasua kasi iongezwe kwani mji unakua ila maji hayajawafikia .
" Eneo la Tamco-Mapinga zaidi ya miaka mitano wapo wananchi walifanyiwa tathmini lakini hawajalipwa fidia zao ,tunaomba utusaidie wananchi hawa waweze kufaidika na fidia hizo"alielezea Koka.Koka alitaja tatizo jingine ni ucheleweshaji wa nishati ya umeme , kasi ni ndogo kufika kwa baadhi ya maeneo na wawekezaji ,ameomba uwafikie maeneo yaliyo katika miradi mbalimbali inayoendelea kutekelezwa.
Hivyo makala MSICHAGUE VIONGOZI MAZEZETA NA MANANGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019-SAMIA
yaani makala yote MSICHAGUE VIONGOZI MAZEZETA NA MANANGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019-SAMIA Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MSICHAGUE VIONGOZI MAZEZETA NA MANANGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019-SAMIA mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/msichague-viongozi-mazezeta-na-mananga.html
0 Response to "MSICHAGUE VIONGOZI MAZEZETA NA MANANGA UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019-SAMIA"
Post a Comment