JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP

JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP
kiungo : JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP

soma pia


JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP

Na Karama Kenyunko, blogu ya Jamii

UPANDE wa mashtaka katika kesi ya uhujumu uchumi inayomkabili mstaafu wa Shirika la Mafuta Tanzania na Zambia (Tazama), Samwel Nyakirang'ani na wenzake 11, umeileza Mahakama ya Hakimu Mkazi Kisutu kuwa Jalada la keai hiyo lipo kwa (DPP), kwa ajili ya kulichambua na kulitolea maamuzi.

Wakili wa Serikali Mwandamizi, Patrick Mwita, ameeeleza hayo leo mbele ya Hakimu Mkazi Mkuu Thomas Simba, kesi hiyo ilipokuja kwa ajili ya kutajwa.Mwita alidai jalada lipo kwa DPP kwa ajili ya kulichambuliwa na kulitolea maamuzi kwa kuangalia washtakiwa gani washtakiwe na washtakiwa gani waachiwe huru na pia itatoa maamuzi kama Mahakama ya Kisutu itapata mamlaka ya kusikiliza kesi hiyo au itahamishiwa Mahakama ya mafisadi.

Ameongeza wapo katika hatua za mwisho za kukamilisha uchambuzi, hivyo wanaomba mahakama yako ipange tarehe nyingine, kwa ajili ya kutajwa.Baada ya kusikiliza hoja hizo, wakili wa utetezi, Alex Balomi ameutaka upande wa mashtaka kuongeza kasi ya ufuatiliaji wa kesi hiyo ili DPP aweze kutoa maamuzi haraka kwa sababu wateja wake wanaendelea kusota mahabusu.

Hakimu Simba ameutaka upande wa mashtaka kuharakisha zoezi la uchambuzi ili haki iweze kupatikana." Upande wa mashtaka mfuatilie kwa DPP kujua anamaliza lini kulipitia faili hili maamuzi yaweze kufanyika na haki iweze kupatikana" alisema Hakimu Simba.

Kesi hiyo imeahirishwa hadi Oktoba 17, 2018. Mshtakiwa Nyakirang’anyi na wenzake katika kesi hiyo wanakabiliwa na mashtaka matatu likiwemo la kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta mali ya (TPA), Washtakiwa wengine katika kesi hiyo ni Nyangi Mataro, mwalimu wa shule ya msingi Ufukoni na mkazi wa Kisiwani Mkajuni Kigamboni. Mfanyabaishara, Farijia Ahmed, mkazi wa Soko Maziwa Kigamboni, Malaki Mathias, mkazi wa Magogoni, Kristomsi Angelus, mkazi wa Soko Maziwa, Fundi Ujenzi Pamfili Nkoronko, mkazi wa Tungi Kasirati na Henry Fredrick, mkazi wa Tungi Kigamboni.

Wengine ni Audai Ismail ambaye ni mkazi wa Kibaha, Chibony Emmanuel, Roman Abdon, Amina Shaban na Zubery Ally.Kwa pamoja wanakabiliwa na mashtaka matatu ya uhujumu uchumi kwa kujiunganishia isivyo halali bomba la mafuta, kinyume cha sheria ya Uhujumu uchumi.


Hivyo makala JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP

yaani makala yote JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/jalada-kesi-tuhuma-za-uhujumu-uchumi.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "JALADA KESI TUHUMA ZA UHUJUMU UCHUMI INAYOMKABILI MSTAAFU WA TAZAMA LIPO KWA DPP"

Post a Comment