DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI.

DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI. - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI., tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI.
kiungo : DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI.

soma pia


DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI.

Kutoka kulia ni Diwani wa Kata ya Kijichi Eliasa Mtarawanje akikabidhi vitabu katika shule ya sekondari kijichi.
Wanafunzi wa shule ya Sekondari Kijichi.
Na Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Diwani wa Kata ya Kijichi amekabidhi vitabu I00 katika shule ya sekondari ya Kijichi iliyopo Manispaa ya Temeke jijini Dar es salaam kwa lengo la kuchangia maendeleo katika sekta ya elimu.

Vitabu hivyo ni msaada kutoka Taasisi isiyokuwa ya Kiserikali ya Pamoja Youth Group  ambapo wametoa msaada baada ya diwani huyo kuomba ili shule ipate vitabu na kufanikisha maendeleo ya elimu.

Masaada huo ni vitabu vya biolojia 80, kiswahili vitabu 20  ambapo imeelezwa lengo kuu ni kuendeleza na  kukuza sekta ya elimu nchini.

Akizungumza leo jijini Dar es Salaam wakati akipokea vitabu hivyo Diwani wa Kata ya Kijichi Eliasa Mtarawanje, amesema kuwa vitabu hivyo vitaongeza chachu ya maendeleo katika shule hiyo kufanya vizuri.

Bw. Mtarawanje amesema kuwa lengo ni  kuunga mkono juhudi za serikali katika utoaji elimu bure ili kufanikiwa kwa asilimia kubwa.

Bw. Mtarawanje ameishukuru taasisi hiyo kwa kuwapatia msaada wa vitabu, ambapo anaamini vitabu hivyo vitakuwa msaada mkubwa kwa wanafunzi wa shule hiyo.

Afisa Elimu wa Kata ya Kijichi Stella John, amefurahishwa na Taasisi hiyo kwa kuonyesha mchango wao wa kuwasaidia vijana katika kuhakikisha wanapata elimu bora.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Taasisi ya Pamoja Youth Group Kassim Mpeta, amesema kuwa lengo la kutoa msaada wa vitabu ni kuendelea kuunga mkono juhudi za serikali ya awamu ya tano katika sekta ya elimu.

Nao wanafunzi wameishukuru taasisi hiyo kwa kupatiwa msaada wa vitabu kwani ni sehemu ya kufanikisha maendeleo katika safari yao ya kupata elimu.

Katika hatua nyengine wamefanya zoezi la upandaji wa miti pamoja na kutolewa elimu ya upandaji wa miti kwa ajili ya kutunza mazingira.


Hivyo makala DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI.

yaani makala yote DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/diwani-kijichi-alivyokusudia-kuwasaidia.html

Subscribe to receive free email updates:

Related Posts :

0 Response to "DIWANI KIJICHI ALIVYOKUSUDIA KUWASAIDIA WANANCHI."

Post a Comment