ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI

ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI - Hallo rafiki WORLD MAELEZO LATEST, Katika makala kusoma wakati huu na kichwa ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI, tumeandaa vizuri kwa makala hii kusoma na kupakua maelezo humo. pengine kujaza posts makala afya, makala biashara, makala general, makala hobby, makala karibuni info, makala michezo, makala siasa, makala utamaduni, sisi kuandika anaweza kuelewa. Naam, furaha ya kusoma.

title : ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI
kiungo : ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI

soma pia


ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI

Image result for picha ya ndalichako
Na Ismail Ngayonga- MAELEZO-DAR ES SALAAM
MAENDELEO  ya jamii yoyote yanahitaji elimu ili wananchi wake waweze kushiriki kikamilifu katika kukabiliana na changamoto zinazowazunguka.
Matarajio ya elimu bora ndani ya jamii yanatokana na mafunzo bora ya walimu ambao ndiyo watendaji wakuu katika mchakato wa kujifunza na kufundisha katika ngazi zote za elimu ya awali, msingi, sekondari na vyuo.
Katika miaka ya hivi karibuni kumekuwepo na jitihada nyingi za Serikali katika kuboresha mazingira ya elimu nchini ikiwemo ongezeko kubwa la idadi ya wanafunzi walio shuleni, ongezeko la madarasa na wingi wa vifaa vya kufundishia na kujifunzia.
Taarifa ya Ofisi ya Rais (Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa-TAMISEMI) inaonyesha kuwa uandikishaji wa wanafunzi wa Darasa la kwanza hadi kufikia machi 2018 ulifikia 1,751,221, pamoja na ongezeko la ajira za walimu wapya wa shule za msingi 2,767 na uhamisho wa walimu wa ziada 8,834 wa sayansi na lugha katika shule za sekondari kwenda shule za msingi.
Pamoja na juhudi hizi kubwa za kuboresha elimu, ubora wa elimu unaendelea kushuka siku hadi siku katika ngazi zote kuanzia shule za msingi, sekondari,  vyuo vya kawaida na hadi Vyuo Vikuu kutunukiwa vyeti wakiwa na maarifa finyu na kushindwa kuchangia kikamilifu maendeleo ya jamii.
Miongoni mwa sababu kubwa inayochangia kushuka kwa kiwango cha elimu nchini ni pamoja na mafunzo duni ya ualimu yanatokana na kupunguzwa kwa muda wa walimu kukaa vyuoni, mitaala ya ualimu kupitwa na wakati na kupotea kwa hamasa kwa walimu.
Katika kukabiliana na changamoto husika, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo imeendelea kutoa mafunzo ya kuwajengea uwezo walimu, wakuu wa shule na Maafisa elimu kuhusu uongozi, uaandaji, usimamizi na ufuatiliaji pamoja na mbinu bora za ufundishaji, kusoma, kuandika na kuhesabu.
Akiwasilisha Hotuba ya Makadirio ya Bajeti ya Mapato na Matumizi kwa mwaka 2018/19, Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia, Prof. Joyce Ndalichako anasema Serikali imeendelea kutoa mafunzo ya muda mrefu na mfupi kwa walimu na viongozi wa elimu, ili kuimarisha uongozi, kutoa ushauri wa kitaalamu katika  maeneo   ya   uongozi   na   uendeshaji wa elimu.
Prof. Ndalichako anasema katika mwaka 2017/18, Serikali kupitia Wakala wa Maendeleo ya Uongozi wa Elimu (ADEM) imedahili walimu 1,831 wakiwemo wanaume ni 1,039 na wanawake ni 792 katika kozi za Stashahada ya Uongozi na Usimamizi wa Elimu na kozi ya Stashahada ya Uthibiti Ubora wa Shule.
Aidha Waziri Ndalichako anasema ADEM pia imedahili Walimu Wakuu 704 wakiwemo wanaume 518 na wanawake 186 kutoka mikoa ya Mbeya, Iringa na Songwe wanaochukua kozi ya Astashahada ya Uongozi, Usimamizi na Utawala katika Elimu.
“Mafunzo hayo yalilenga kutoa elimu katika maeneo ya Usimamizi na Utawala wa Shule, Ushauri na Unasihi, Utekelezaji wa Sera za Elimu, Udhibiti wa Majanga shuleni, Mfumo wa Usimamizi wa Utendaji Kazi, Ufuatiliaji na Tathmini ya Mipango ya Shule, Usimamizi wa Rasilimali za Shule” anasema Prof. Ndalichako.
Kwa mujibu wa Prof. Ndalichako anasema katika mwaka 2017/18, ADEM pia umefanya ukarabati wa mabweni 2 yenye uwezo wa kuchukua wanachuo 450 na kumbi 2 za mihadhara zenye uwezo wa kuchukua wanachuo 150 kila mmoja pamoja na kukamilisha michoro kwa ajili ya ujenzi wa  Kampasi  za  Mbeya na Mwanza zitakazokuwa na uwezo wa kudahili wanachuo 700.
Anaongeza kuwa kupitia ADEM, Serikali pia imeratibu uendeshaji wa mafunzo kwa walimu 1,568 wa vituo vya Ualimu Nje ya Mfumo Rasmi (MEMKWA) yenye lengo la kuimarisha Stadi za Kusoma, Kuandika na Kuhesabu.
Katika hatua nyingine, Profesa Ndalichako anasema Serikali ya Tanzania kwa kushirikiana na Serikali ya Canada zinatekeleza mradi wa  Ukarabati wa Vyuo vinne vya Ualimu vya Ndala, Shinyanga, Kitangali na Mpuguso unalenga kuboresha miundombinu na mazingira ya kufundishia na kujifunzia.
Anasema kupitia mradi huo, Serikali imekamilisha ujenzi wa jengo la nyumba za walimu la ghorofa 2 kwa ajili ya familia 4 ambalo tayari limekabidhiwa katika Chuo cha Ualimu Shinyanga, pamoja na kuendelea na ujenzi wa majengo 2 ya bweni yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 152 kila moja na ujenzi wa uzio ambao umekamilika kwa asilimia 90.
Akifafanua zaidi Ndalichako anasema Serikali pia imeendelea na ujenzi wa mabweni mawili katika Chuo cha Ualimu Mpuguso yenye uwezo wa kuchukua wanafunzi 308, nyumba za walimu majengo 3 ya ghorofa, ambavyo kwa pamoja  kwa ujumla vimekamilika kwa asilimia 85.
Serikali imekusudia kuleta mapinduzi ya kiuchumi ili kuibadili Tanzania kuwa nchi ya uchumi wa kati ifikapo mwaka 2025 kwa kutayarisha idadi ya kutosha ya Watanzania walioelimika na kupenda kujielimisha.
Ili kufikia malengo hayo, Serikali na wadau wa maendeleo hawana budi kuzalisha raslimali watu wenye ujuzi kulingana na mahitaji yaliyopo.


Hivyo makala ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI

yaani makala yote ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.

Wewe ni sasa kusoma makala ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/10/adem-taswira-ya-maendeleo-ya-sekta-ya.html

Subscribe to receive free email updates:

0 Response to "ADEM TASWIRA YA MAENDELEO YA SEKTA YA ELIMU NCHINI"

Post a Comment