title : WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI
kiungo : WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI
WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI
Na Veronica Kazimoto ,Dar es Salaam
Hivi karibuni Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kupitia Mamlaka ya Mapato Nchini (TRA) ilitoa msamaha maalum wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 50 ya hapo awali.
Msamaha huu umetokana na malalamiko ya wafanyabiashara waliyoyatoa kwa Mhe. Rais Dk. John Pombe Joseph Magufuli ya kuwepo kwa malimbikizo makubwa ya madeni ya kodi za nyuma yakijumuisha riba na adhabu wakati wa Mkutano wa 11 wa Baraza la Taifa la Biashara (TNBC) uliofanyika Ikulu jijini Dar es Salaam mnamo tarehe 19 Machi, 2018.
Kufuatia malalamiko hayo, Rais aliwaambia wafanyabiashara hao kuzungumza na Wizara ya Fedha na Mipango ili waweze kupunguziwa riba na adhabu za madeni yao ya kodi.
"Suala la kodi ni very sensitive (nyeti sana) hata Rais unaweza kushtakiwa kwa kukwepa kodi, mimi niwaombe wale mnaodaiwa kwa miaka ya nyuma nendeni mka-negotiate (mkajadiliane) na Wizara ya Fedha, ninajua kuna kipengele ambacho kinaweza kuwapunguzia", alisema Rais Magufuli.
Dk. Magufuli alitumia baraza hilo pia kuwasisiza wafanyabiashara kulipa kodi ambapo alisema "Tunahitaji kodi kwa ajili ya survival (kudumu) ya nchi hii, mtu ajue kwamba kulipa kodi ni wajibu wake na kukwepa kodi is a big crime (kosa kubwa). Hivyo ninawaomba wafanyabiashara msikwepe kulipa kodi, mjitahidi kulipa kwa maana kodi hizi ndio zinatusaidia kuijenga nchi yetu".
Baada ya mkutano huo wa baraza la biashara, Bunge la Tanzania katika kikao chake cha bajeti cha Mwaka wa Fedha 2018/19 cha mwezi Juni, 2018 lilipitisha marekebisho ya Kifungu cha 70 cha Sheria ya Usimamizi wa Kodi ya Mwaka 2015 ili kumpa mamlaka Waziri mwenye dhamana ya Fedha ya kutunga kanuni maalum za kutoa msamaha wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi ya nyuma.
Kupitia marekebisho hayo, Waziri wa Fedha na Mipango, alimpa Mamlaka Kamishna Mkuu wa TRA kutoa msamaha maalum wa riba na adhabu kwenye malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 tofauti na asilimia 50 ya awali.
Ni kufuatia mamlaka hayo, Kamishna Mkuu wa TRA Charles Kichere alitangaza msamaha huo maalum mnamo tarehe 11 Julai, 2018 kwa lengo la kutoa unafuu kwa walipakodi wenye malimbikizo ya madeni ya riba na adhabu kwa kuwapa fursa ya kulipa kodi ya msingi (principal tax) mara moja au kwa awamu ndani ya mwaka wa fedha wa 2018/19.
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) Charles Kichere akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati akitangaza msamaha maalum wa riba na adhabu ya malimbikizo ya madeni ya kodi kwa asilimia 100 jijini Dar es Salaam Julai, 2018. Kushoto kwake ni Mkurugenzi wa Huduma na Elimu kwa Mlipakodi wa Mamlaka hiyo Richard Kayombo.
Hivyo makala WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI
yaani makala yote WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/wafanyabiashara-changamkieni-msamaha-wa.html
0 Response to "WAFANYABIASHARA CHANGAMKIENI MSAMAHA WA RIBA NA ADHABU YA KODI"
Post a Comment