title : UWEKEZAJI AWAMU YA PILI YA KIWANDA CHA VIATU -KARANGA KUGHARIMU BIL 67
kiungo : UWEKEZAJI AWAMU YA PILI YA KIWANDA CHA VIATU -KARANGA KUGHARIMU BIL 67
UWEKEZAJI AWAMU YA PILI YA KIWANDA CHA VIATU -KARANGA KUGHARIMU BIL 67
Na Dixon Busagaga,Moshi.
MRADI wa Kiwanda cha kutengeneza Viatu cha Karanga Leather Industries Co.Ltd upo katika hatua ya mwisho kukamilika baada ya kufanyika maboresho katika ufungaji wa mitambo mipya ya kukata na kushona ngozi pamoja na mfumo wa umeme katika kiwanda hicho.
Kampuni inayosimamia Kiwanda cha kutengeneza Viatu cha Karanga -Moshi, ilianzishwa Mei 30 mwaka jana kwa ubia kati ya uliokuwa Mfuko wa Hifadhi ya Jamii PPF na Jeshi la Magereza ,ambapo awali kilikuwa kikizalisha jozi 150 kwa siku.
Baada ya Maboresho kukamilika kiwanda hicho sasa kitaweza kuzalisha Jozi 400 kwa siku na kutokana na sasa kuweza kuweka soli za viatu,kushona ngozi na kazi nyingine.Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza nchini ,Phaustine Kasike pamoja na Kaimu Mkuu wa Mkoa wa Kilimanjaro ,Onesmo Buswelu wametembelea Kiwanda hicho kujionea maboresho hayo ambayo yanakadiliwa kufikia kiasi cha Sh Bil 2.7 katika uwekezaji wa Mitambo na kuoneshwa kuridhishwa.
Akizungumza na waandishi wa Habari mara baada ya kutembelea Kiwanda hicho,kamishna Jenerali Kasike amesema ujenzi wa miradi hiyo miwili pamoja na utekelezaji wa agizo la Rais kuwa na Tanzania ya Viwanda ,lakini pia itaongeza ajira na kuwawezesha wafungwa kuwa na ujuzi ambao watautumia kuajiri na kujiajiri baada ya kutukimikia kifngo.
Kamishana Jenerali wa Magereza,Phaustine Kasike pamoja na Kaimu Mkuu wa mkoa wa Kilimanjaro,Onesmo Buswelu (mwenye suti katikati) wakipata maelezo kutoka kwa Mkuu wa Kiwanda cha Viatu-Karanga,Ezron Nganoga.
Kamisha Jenerali wa Magereza akitizama bidhaa za viatu ambazo zilinazalishwa katika kiwanda cha Viatu cha Karanga kinachomilikiwa kwa ubia kati ya uliokuwa mfuko wa Hifadhi ya Jamii (PPF) na Jeshi la Magereza.
Kamishna Jenerali wa Jeshi la Magereza ,akiizama bidhaa mbalimbali za Viatu zinazozalishwa na kiwanda hicho.
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
KUSOMA ZAIDI BOFYA HAPA>>>>>>
Hivyo makala UWEKEZAJI AWAMU YA PILI YA KIWANDA CHA VIATU -KARANGA KUGHARIMU BIL 67
yaani makala yote UWEKEZAJI AWAMU YA PILI YA KIWANDA CHA VIATU -KARANGA KUGHARIMU BIL 67 Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala UWEKEZAJI AWAMU YA PILI YA KIWANDA CHA VIATU -KARANGA KUGHARIMU BIL 67 mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/uwekezaji-awamu-ya-pili-ya-kiwanda-cha_3.html
0 Response to "UWEKEZAJI AWAMU YA PILI YA KIWANDA CHA VIATU -KARANGA KUGHARIMU BIL 67"
Post a Comment