title : TARA WAKUTANA DAR KUTAFUTA UDHIBITI WENYE VIWANGO.
kiungo : TARA WAKUTANA DAR KUTAFUTA UDHIBITI WENYE VIWANGO.
TARA WAKUTANA DAR KUTAFUTA UDHIBITI WENYE VIWANGO.
Mkurugenzi wa Jumuia ya Nchi zenye Reli Kusini mwa Afrika (TARA), Babe Botana Akizungumza na waandishi wa habari leo jijini Dar es Salaam katika Mkutano kutafuta maadhimio ya viwango sawa katika kudhibiti ubora.
Picha ya reli.
Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Jumuia ya Nchi zenye Reli kusini mwa afrika (TARA) zimetakiwa kuwa na ushirikiano ili kuhakikisha zinakuwa na viwango sawa vya kudhibiti usalama.
Katika kufanikisha mpango huo nchi hizo ikiwemo Tanzania, Malawi, Msumbiji wamefanya mkutano wa pamoja ili kupata maadhimio yenye lengo la kuleta muunganiko wa pamoja katika viwango sawa vya kudhibiti.
Kwa sasa nchi mbili Tanzania na South Afrika ndio zinazothibiti usalama wa huduma za reli katika kiwango sawa.
Akizungumza na waandishi wa habari leo, jijini Dar es Salaam, Katibu Mkuu wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano Mhandisi Dk. Leonard Chamuriho, amesema kuwa kutokana na changamoto ya udhibiti wa usalama nchi za Jumuia ya Maendeleo ya Nchi za afrika ya kusini (SADC) zimekutana ili kuhamasisha nchi nyengine kuwa na usalama katika kutoa huduma.
Amesema kuwa lengo la mkutano huo kwa ajili ya kuhamasisha nchi nyengine ziwe na usalama katika viwango sawa.
Dkt. Chamuriho ameeleza kuwa katika mkutano huo wanategemea kupata maadhimio ya jinsi ya kuungana au kupata udhibiti wenye kiwango kimoja.
"Mfano unakuta treni moja inatoka South afrika hadi Dar es Salaam, lakini inapopita nchi nyengine kunakuwa na udhibiti tofauti" amesema Dkt. Chamuriho.
Mkurugenzi wa Mamlaka ya Usafiri wa nchi kavu na majini (SUMATRA), Giliard Ngewe, amesema kuwa tusipokuwa na udhibiti unaofafana ni laziwa viwango vitofautiane.
Amesema kuwa ni vizuri tukawa na viwango sawa ili kuhakikisha usalama katika reli zetu.
Hivyo makala TARA WAKUTANA DAR KUTAFUTA UDHIBITI WENYE VIWANGO.
yaani makala yote TARA WAKUTANA DAR KUTAFUTA UDHIBITI WENYE VIWANGO. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala TARA WAKUTANA DAR KUTAFUTA UDHIBITI WENYE VIWANGO. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/tara-wakutana-dar-kutafuta-udhibiti.html
0 Response to "TARA WAKUTANA DAR KUTAFUTA UDHIBITI WENYE VIWANGO."
Post a Comment