title : PROF. NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI
kiungo : PROF. NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI
PROF. NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako akizungumza na wataalmu wa somo la Hisabati katika kongamano la tano la Hesabu lililofanyika nchini kwa kuandaliwa na Chuo Kikuu cha Agha Khan.
Na Humphrey Shao, Globu ya Jamii
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi, Profesa Joyce Ndalichako amesema Serikali imejipanga kuhakikisha Walimu wa Somo la Hisabati nchini wanaongezeka hili kuweza kukidhi mahitaji ya walimu hao katika shule za Msingi na Sekondari.
Profesa Ndalichako amesema hayo alipokuwa akifungua Kongamano la tano la Wakufunzi wa Hisabati kutoka sehemu mbalimbali barani Afrika lililoandaliwa na Chuo Kikuu cha Agha Khan hapa nchini.
“Mkutano huu umekutanisha wataalamu kutoka Afrika na Nje ya Afrika kwa lengo la kuongeza jitihada za kuimarisha mbinu za ufundishaji wa Hisabati , hivyo tunataka kuongeza walimu wa hesabu hapa nchini lakini tumekuwa na upungufu wa vijana wanaomaliza elimu yao ya sekondari ambao ni wataalamu wa Hisabati hivyo nyie muende kuhamasisha vijana wakapende hesabu hili tuweze kupata mzunguko mzuri wa wataalamu wa hesabu kila mwaka”amesema Ndalichako.
Amesema hali ya uchache wa utayari wa vijana wanaojitokeza kuja kusoma hesabu imekuwa chanzo cha upungufu wa walimu wa somo hilo nchini hivyo Serikali ipo katika mpango kabambe wa kuhamasisha watoto wakasoma hesabu na kufanya vizuri katika masomo yao wakiwa darasani.
Waziri Ndalichako amesema kuwa ukiboresha ufundishaji wa somo la hesabu utasaidia kuboresha masomo mengine kwani masomo mengi yanategmea utalaamu wa hesabu kufanikisha ufaulu.
Ameongeza kuwa Serikali imejipanga kupokea maoni ni namna gani itaweza kuboresha mfumo wa utoaji wa elimu hasa kwa somo la hesabu hili kuweza kuongeza ufaulu katika shule za serikali.
Ametaja kuwa Serikali ya awamu ya tano inayoongozwa na Rais Dr John Pombe Magufuli imeweza kuleta mfumo wa elimu bure kwa kutoa elimu ya kiwango cha hali ya juu na sio bora elimu hivyo walimu ni vyema wakathamini mchango unaotolewa na serikali ya awamu ya tano kwa wanafunzi kwa kumuunga mkono Rais wetu.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akisalimiana na baadhi ya magwiji wa Hesabau waliofika katika mkutano huo.
Sehemu ya Washiriki wakiwa katika Ukumbi wa Mkutano wa Chuo Kikuu cha Agha Khan wakisikiliza hotuba ya Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako.
Waziri wa Elimu na Mafunzo ya Ufundi Profesa Joyce Ndalichako akiwa katika picha ya pamoja na Washiriki wa Kongamano hilo
Hivyo makala PROF. NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI
yaani makala yote PROF. NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala PROF. NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/prof-ndalichako-serikali-imejipanga.html
0 Response to "PROF. NDALICHAKO; SERIKALI IMEJIPANGA KUONGEZA WALIMU WA SOMO LA HESABU NCHINI"
Post a Comment