title : NSSF KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI SIMIYU
kiungo : NSSF KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI SIMIYU
NSSF KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI SIMIYU
Shirika la la Taifa la Hifadhi ya jamii NSSF linashiriki kwenye maonesho ya wakulima NANE NANE yaliyoanza tarehe moja mwezi wa nane katika viwanja vya Nyakabunda mkoani Simiyu.
Kaimu meneja Uhusiano na Masoko wa NSSF Salim Khalfan amesema kuwa mwaka huu wameshiriki tena ambapo amewataka wananchi kujitokeza kwa wingi kwenye banda lao kwa ajili ya kujua masuala mbali mbali.
“Tumejipanga vyema kwenye maonesho ya mwaka huu, tunaomba wananchi wajitokeze kwa wingi katika banda letu kujionea mambo mbali mbali tynayoyafanya ” Khalfan amesema kuwa katika banda la NSSF wananchi wataweza kupata elimu juu ya mafao yanayotolewa na Shirika kama vile mafao ya matibabu ambayo kwa kiasi kikubwa yamesaidia sana kuimarisha sekta ya afya hapa nchini.
Pia amesema kuwa kutakuwepo na zoezi la uandikishaji kwa wananchi ambao wako kwenye sekta isiyo rasmi na wataweza kujiunga na NSSF kufaidika na mafao yanayotolewa. “Kutakuwepo na zoezi la kuandikisha wanachama wapya kwenye maonesho hayo ya nanenane hivyo ni wakati pekee kuja kujiandikisha “Alisema Khalfan.
Tunapoazimisha sikukuu ya wakulima nchini ,NSSF inatoa fursa mbali mbali kwa wakulima zikiwemo mkulima kuweza kujiandikisha na kuchangia kwa kiasi cha shilingi elfu ishirini tu kila wmezi na kufaidika na mafao yanayotolewa baada ya kukidhi sifa stahili za kuwa mwananchama wa Hiari.
Huu ni muendelezo wa Shirika la NSSF kushiriki katika maonesho ya wakulima ya nane nane ambayo kwa namna moja ama nyingine yanasaidia kutangaza fursa mbali mbali kwa wakulima nchini.
Imetolewa na Kitengo cha Uhusiano na Masoko
Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii NSSF
Hivyo makala NSSF KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI SIMIYU
yaani makala yote NSSF KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI SIMIYU Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala NSSF KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI SIMIYU mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/nssf-kushiriki-maonesho-ya-wakulima.html
0 Response to "NSSF KUSHIRIKI MAONESHO YA WAKULIMA NANE NANE MKOANI SIMIYU"
Post a Comment