title : Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Wakabidhi Magari Matatu kwa Ajili ya Wanafunzi na Shughuli za Kijamii Jimboni.
kiungo : Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Wakabidhi Magari Matatu kwa Ajili ya Wanafunzi na Shughuli za Kijamii Jimboni.
Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Wakabidhi Magari Matatu kwa Ajili ya Wanafunzi na Shughuli za Kijamii Jimboni.
MAGARI matatu yakionekana pichani yaliyotolewa na Mbunge wa Kijitoupele na Pangawe Shamsi Vuai Nahodha.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘’Mabodi’’ akikata utepe wa kuzinduliwa rasmi kwa magari hayo ambayo ni mabasi mawili ya Wanafunzi wa Majimbo hayo na Canter moja kwa ajili ya shughuli za kijamii.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘’Mabodi’’ akiendesha gari aina ya Canter iliyotolewa na Mbunge huyo.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘’Mabodi’’ akikagua maendeleo ya ujenzi wa Skuli ya msingi ya Kwarara inayojengwa na viongozi wa jimbo hilo.
MBUNGE wa majimbo ya Kijitoupele na Pangawe, Shamsi Vuai Nahodha akizungumza katika hafla hiyo ya makabidhiano ya Maghari hayo.
NAIBU Katibu Mkuu wa CCM Zanzibar Dk. Abdulla Juma Saadalla ‘’Mabodi’’ akizungumza na wananchi wa majimbo ya Kijitoupele na Pangawe katika hafla ya kuwakabidhi magari matatu ambayo ni mabasi mawili na Canter moja yaliyotolewa na Mbunge wa Majimbo hayo Shamsi Vuai Nahodha.
Na. Is-Haka Omar, Zanzibar.
NAIBU Katibu Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi(CCM)
Zanzibar, Dk.Abdulla Juma Mabodi amewataka Wabunge na
Wawakilishi nchini kuongeza kasi ya kutatua kero za
wananchi kwa wakati kama walivyowaahidi katika kampeni
za uchaguzi mkuu uliopita.
Kauli hiyo ameitoa mara baada ya kukabidhi magari matatu
kwa wananchi wa majimbo ya Kijitopele na Pangawe
ambapoMagari hayo yana thamani ya shilingi milioni 128
yaliyotolewa na Mbunge wa Majimbo hayo, Shamsi Vuai
Nahodha.
Akizungumza katika ziara yake ya kutembelea majimbo
hayo iliyofanyika katika uwanja wa mpira wa Magirisi
uliopo Kijitoupele, Dk.Mabodi alisema huu ndio wakati wa
viongozi wa majimbo kutekeleza kwa kasi Ilani ya Uchaguzi
ya mwaka 2015/2020.
Akizungumzia vitendea kazi hivyo ambavyo ni magari
matatu yakiwemo mabasi ya Wanafunzi mawili na moja
ambalo ni Canter kwa ajili ya shughuli za kijamii, aliwambia
wananchi kuwa wanakiwa kuthamini juhudi za kiongozi
huyo aliyetekeleza ahadi yake kwa vitendo.
Dk. Mabodi alieleza kwamba malengo ya Chama Cha
Mapinduzi ni kuhakikisha wananchi wa mijini na vijijini
wanaondokana na changamoto mbali mbali za kijamii kabla
ya uchaguzi mkuu ujao.
Alisema mabasi yaliyotolewa yatawasaidia wanafunzi wote
wa majimbo hayo bila kujali tofauti za kisiasa.
kiongozi huyo A katika ziara yake ya kutembelea miradi
mbali mbali ya Chama iliyokutekeleza ahadi walizowaahidi
wananchi katika kampeni amesema wananchi wanakiamini
na kukiunga mkono Chama kutokana na kutatua kwa wakati
kero zinazowakabili wananchi.
“Miradi mbali mbali ya maendeleo inayotekelezwa
majimboni na viongozi wa CCM ni kwa ajili ya wananchi
wote, na tunaomba wananchi muendelee kutuamini na
hatimaye mwaka 2020 mkichague Chama chetu kiendelee
kuongoza dola.”, alisema Dk. Mabodi.
Naye Mbunge wa majimbo hayo, Shamsi Vuai Nahodha
alisema CCM imeendelea kuwa na mvuto kwa jamii
kutokana na ukweli na dhamira ya dhati ya viongozi wake
kuwatumikia wananchi kwa vitendo.
Mbunge huyo Naohodha ambaye pia ni Waziri Kiongozi
Mstaafu wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar alisema kwa
kushirikiana na viongozi wengine wa majimbo mawili
anayoyatumikia wamefanikiwa kutatua kero za wananchi
kwa kiwango kikubwa.
Shamsi alisema na kuongeza kuwa wameimarisha huduma
muhimu za kijamii zikiwemo upatikanaji wa maji safi na
salama, ujenzi wa vituo vya Afya pamoja na ujenzi wa shule
za kisasa za msingi na sekondari.
Katika ziara hiyo Naibu Katibu Mkuu pia alitembelea ujenzi
wa Kituo cha Afya katika Jimbo la Kijitoupele ambacho
kimejengwa kwa ushirikiano wa Mwakilishi wa jimbo hilo,
Ali Suleiman Ali ‘’Shihata’’ pamoja na Mbunge wa jimbo hilo
Shamsi Vuai Naohodha ambacho hadi kukamilika kwake
kitatumia zaidi ya shilingi milioni 59.
Pia Naibu Katibu Mkuu Dk. Mabodi alitembelea Shule ya
Sekondari Kwarara na Kituo cha elimu na habari sambamba
na kukagua ujenzi wa shule ya msingi ya Kwarara
itakayotumia shilingi bilioni 1.3 hadi ujenzi wake kukamilika.
Hivyo makala Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Wakabidhi Magari Matatu kwa Ajili ya Wanafunzi na Shughuli za Kijamii Jimboni.
yaani makala yote Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Wakabidhi Magari Matatu kwa Ajili ya Wanafunzi na Shughuli za Kijamii Jimboni. Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Wakabidhi Magari Matatu kwa Ajili ya Wanafunzi na Shughuli za Kijamii Jimboni. mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mbunge-na-mwakilishi-wa-jimbo-la.html
0 Response to "Mbunge na Mwakilishi wa Jimbo la Pangawe na Kijitoupele Wakabidhi Magari Matatu kwa Ajili ya Wanafunzi na Shughuli za Kijamii Jimboni."
Post a Comment