title : MASHINDANO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI YAPAMBA MOTO
kiungo : MASHINDANO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI YAPAMBA MOTO
MASHINDANO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI YAPAMBA MOTO
Wanafunzi wa kidato cha sita Pilly Ndobeji pamoja na Naomi Shanguya kutoka shule ya Sekondari Pandahili iliyopo Mkoani Mbeya wakionyesha kazi yao ya kisayansi ambapo wamegundua dawa ya kuuwa wadudu wanaruka.Wananafunzi hao wanasomba mchapuo wa PCB wanamalengo ya kuja kuwa wana sayansi wakubwa barani afrika.
Kutoka kushoto ni Mwanafunzi wa kidato cha tatu Arafati Shabani kutoka shule ya sekondari ya Kitongoni Mkoani Kigoma akiwa na mwezake Busogo Busogo akielezea kazi yao ya kisayansi waliogundua.
Katika maelezo yao wamegundua utofauti kati ya Sodium and Potassium Hydroxide Solution baada ya kufanya majaribio(experiment).
Noel Rukanuga, Dar es Salaam.
Zaidi ya wana sayansi chipukizi 200 kutoka shule za sekondari wamekutana jijini Dar es Salaam katika maonyesho ya nane kwa ajili ya kushindanisha kazi zao za kisayansi ambazo zimelenga kuleta hamasa kwa wanafunzi kupenda masomo ya sayansi.
Akzungumza na mwandishi wa habari jijini leo jijini Dar es Salaam Mwanjilishi mweza wa Shirikisho la Wanasayansi Chipukizi Tanzania Dkt. Gozibert Kamugisha, amesema kuwa maonyesho hayo yamelenga kuleta hamasa kwa wanafunzi ili kuhakikisha wanapenda masomo ya sayansi.
Dkt. Kamugisha amesema kuwa katika maonyesho ya mwaka huu wanafunzi wa shule za sekondari wanashindana kupitia kazi zao za kisayansi ambazo zimelenga kuisaidia jamii.
Amesema kuwa kuna makundi tofauti ambayo yanashindana ikiwemo katika hesabu, Bailojia na chemia.
"Kuna category tofauti..lakini washindi katika kila category watapata zawadi kuanzia Milioni moja na kuendelea na wanafunzi wanne waliofanya vizuri watasomeshwa bure elimu ya shahada ya kwanza" amesema Dkt. Kamugisha.
Amefafanua kuwa maonyesho hayo yametoa fursa kwa wanafunzi kuonyesha uhusiano wao na kile walichokisoma darasani kwa njia ya vitendo.
Ameeleza kuwa kupitia vipaji vya wana sayansi chipukizi walivyogundua kunaweza kuleta mabadiliko chanya katika kutatua changamoto katika jamii.
"Kizazi cha wana sayansi chipukizi kinategemewa sana katika kufanya vizuri miaka ijayo" amesema Dkt. Kamugisha.
Hata hivyo ameeleza ipo mipango ya kuwaendeleza wanafunzi ambao wameonekana wanavipaji ambapo watashirikiana na wizara mbalimbali ikiwemo wizara ya elimu, Tamisemi, Viwanda.
Hivyo makala MASHINDANO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI YAPAMBA MOTO
yaani makala yote MASHINDANO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI YAPAMBA MOTO Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala MASHINDANO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI YAPAMBA MOTO mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/mashindano-ya-wanasayansi-chipukizi.html
0 Response to "MASHINDANO YA WANASAYANSI CHIPUKIZI YAPAMBA MOTO"
Post a Comment