title : Fichueni wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi-Jaffo
kiungo : Fichueni wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi-Jaffo
Fichueni wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi-Jaffo
Na Chalila Kibuda, Globu ya Jamii
WAZIRI wa Nchi Ofisi ya Rais (TAMISEMI )Selemani Jaffo amewaagiza Wakuu wa Mikoa na Makatibu Tawala walioapishwa na Rais Dk. John Magufuli wakasimamie miradi yote ya serikali na kuwafichua wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi zinazotengwa na serikali.
Pia ametoa siku 10 kwa mikoa yote ambayo bado haijawasilisha mpaka leo ripoti ya Mkaguzi wa Hesabu za Serikali (CAG) kwasilisha katika siku hizo ili shughuli zingine za maendeleo ziendelee.
Amsema bado wapo watendaji wanafanya kazi kwa mazoea kwa kura fedha ya serikali bila ya wogo wowote ni lazima wawajibike wanaofanya hivyo kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala kuwafichua walafi hao.
Jaffo amesema serikali imeweka vipaumbele vyake katika baadhi ya sekta kama vile, Sekta ya afya, elimu na barabara hivyo amewataka wateule hao wakasimamie miradi hiyo ambayo ina umuhimu mkubwa kwa wananchi.
Hayo aliyasema Jafo wakati alipokutana na Wakuu wa Mikoa Wapya na Makatibu Tawala Mikoa mara baada ya kuapishwa na kuwataka kufanya kazi kwa uadilifu na kuwa na nidhamu ya muda na kujua kila mtu mipaka yake
Amesema wadhifa waliopewa ni mkubwa hivyo kila wakati wanatakiwa wanyamazishe vilio vya wananchi pale wanapopata na changamoto ya aina yeyote.
“Hakunba atakayenyamazisha kelele za wananchi isipokuwa ni Wakuu wa Mikoa pamoja na Katibu Tawala “alisema Jaffo.
Pia alisema katika suala la elimu kila shule ya msingi na sekondari inatakiwa kuwa na walimu wa kutosha na kusiwe na walimu wachache na sehemu nyingine kuwe na walimu wengi.
Akizungumzia miundombinu ya barabara alisema, Tanzania inaingia katika mfumo wa viwanda hivyo mfumo wa barabara kwa mijini na vijijini unatakiwa kukamilika ili viwanda viweze kufanya kazi yake vile inavyoitakiwa.
“Maagizo hayo yote ni ya kwenu hivyo mnatakiwa muyachukue ili mukayafanyie kazi vile inavyotakiwa kufanywa”alisema.
Vilevile ,aliwataka viongozi hao waache utamaduni wa kukaa ofisini na badala yake watembelee miradi yote inayosimamiwa na Halmashauri ili kuondoa ubadhirifu .
Wakati huo huo,Katibu Mkuu wa TAMISEMI Injinia Musa Iyombe ,aliwataka Wakuu wa Mikoa hiyo wafanye kazi kwa kufuata maadili yanavyotaka.
“Katika ufanyaji wenu wa kazi msivuke mipaka mtaanza kuleta shida ,ni lazima kila kiongozi asome mipaka yake ya kazi “alisema Iyombe
Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais (Tamisemi)Selemani Jaffo akizungumza wakuu wa mikoa wapya pamoja na makatibu tawala mara baada ya kuapishwa kwa ajili ya kuwapa misingi ya kufanya kazi katika vituo vyao katika hafla iliyofanyika Ofisi za Tamisemi jijini Dar es Salaam.
Naibu Waziri wa Ofisi ya Rais Tamisemi, Josephat Kandege akizungumza namna ya kushughulika katika miundombinu ya mikoa katika mkutano wa wakuu wa mikoa wapya pamoja na makatibu Tawala iliyofanyika katika Ofisi za Tamisemi jijini Dar es Salaam.
Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tamisemi, Mhandisi Mussa Lyombe akizungumza juu ya mipaka ya kazi kwa wakuu wa mikoa na makatibu tawala wapya katika iliyofanyika katika Ofisi za Tamisemi jijini Dar es Salaam.
Baadhi ya wakuu wa Mikoa wapya waliopishwa
Baadhi ya Makatibu Tawala walioapishwa
Hivyo makala Fichueni wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi-Jaffo
yaani makala yote Fichueni wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi-Jaffo Wakati huu, pengine unaweza kutoa faida na wewe wote. Sawa, kuona katika post nyingine makala.
Wewe ni sasa kusoma makala Fichueni wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi-Jaffo mahali kiungo https://wordmaelezo.blogspot.com/2018/08/fichueni-wale-wote-wanaofanya-ujanja.html
0 Response to "Fichueni wale wote wanaofanya ujanja katika fedha za miradi-Jaffo"
Post a Comment